Mwandishi
wa habari wa gazeti la The Citizen na Mwananchi mkoani Singida,Awila
Silla, alipokuwa wodini katika hospitali ya mkoa mjini Singida Septemba 9
mwaka 2013, baada ya kucharangwa mapanga na kisha kuporwa mali
mbalimbali zikiwemo simu mbili za kiganjani.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
KESI
ya unyang’anyi wa kutumia silaha dhidi ya mwandishi wa habari wa
magazeti ya MWANANCHI na THE CITIZEN mkoani Singida, inayomkabil Adamu
Abdallah mkazi wa Utemini mjini Singida, inatarajiwa kutolewa hukumu
yake Desemba 10 mwaka huu.
Mwandishi
wa habari, aliyecharangwa mapanga na kisha kunyang’anywa mali
mbalimbali ikiweno simu mbili za kiganjani, ni Awila Silla mkazi wa
Utemini mjini Singida.
Kesi hiyo no.240/2013 ipo chini ya hakimu mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida, Joyce Minde.
Minde
amesema kuwa ushahidi wa pande zote mbili ambazo ni upande wa jamhuri
na ule wa utetezi, umeishakamilisha utoaji wa ushahidi na hivyo
umefungwa.
Inadaiwa
kwamba Septemba nane mwaka 2013 saa mbili usiku huko maeneo ya Utemini
jirani na mahakama ya mwanzo Utemini, mshitakiwa Adamu alimvamia
mwandishi wa habari Awila,na kumshambulia kwa panga sehemu za usoni na
kumsababishia maumivu makali yaliyopelekea kulazwa katika hospitali ya
mkoa mjini hapa.
Amedaiwa
lengo la mshitakiwa Adamu kumshambulia Awila, ni kumtisha na
kumdhoofisha ili aweze kutekeleza azma yake bila ya matatizo yo yote,
ambapo alifanikiwa kunyang’anya mali mbalimbali na simu mbili moja ikiwa
ni ya aina ya ‘airtel pink.
Pamoja
na mshitakiwa Adam, mshitakiwa namba mbili Muksin Abubakari mkulima na
mkazi wa kijiji cha Kinyeto manispaa ya Singida,ambaye anashitakiwa kwa
kosa la kupatikana na mali ya wizi (simu ya kiganjani mali ya Awila
Silla aina ya airtel pink),hukumu yake inatarajiwa kutolewa desemba 10
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment