Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Katavi Joseph Shilinde akiwasilsha Taarifa ya hali ya ukaguzi wa magari kwenye kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi. |
Kati ya
Mabasi 20 ya abiria yanayotoa huduma ya Usafiri Mkoani Katavi kwenda mikoani ni
basi moja tu linalofanya safari zake Mpanda Arusha la Costal line lenye namba T 467 APZ ndilo ambalo nzima.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani
Katavi Kamanda Joseph Shilinde alikieleza kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa
kilichofanyika mwishoni mwa wiki kuwa kati ya Mabasi hayo mabasi 17 yanemekutwa
na makosa madogodogo yameagizwa kufanyiwa marekebisho.
Kamanda
Shilinde alieleza kuwa Mabasi mawili yameonekeana hayafai kuwa barabarani na
yamefungiwa hadi hapo yatakapokuwa yamefanyiwa matengenezo ameyataja mabasi
hayo ambayo hayafai ni basi lenye
usajiri wa Na AT 664 na T801 ND limefungiwa miezi miwili hadi hapo yatakapokuwa
yamefanyiwa matengenezo.
Mmoja wa
wajumbe katika Kiao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Enock
Gwambasa alieleza kuwa pamoja na ukaguzi huo bado hayajatajwa mabasi ya Kampuni
ya Sumri ambayo inatoa huduma zake kati ya Sumbawanga na Katavi yameelezwa kuwa
ni mabovu kuliko kawaida na yanavuja hata unapoingia humo hayana hata madirisha
kwa wastani mabasi hayo ni mabovu sana ,
Akashangazwa
na kutokuwemo kwenye orodha ya mabasi yaliyotajwa kuwa ni mabovu na kwa namna
gani hayajatajwa katika taarifa hiyo.
Kwa Upande
wake Charles Kanyanda alishauri Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama Barabarani
kuhakikisha suala la Mwendo kasi kwa mabasi yanayofanya safari zake Mkoani
Katavi kutoka Mikoa mingine hali ambayo yansababisha ajali kutokana na barabara
zilizoko kwenye mkoa huu kutokuwa nzuri.
Akasisitiza sheria
za usalama barabara zifuatwe ili kuepusha ajali zisizokuwa na sababu. Ambazo
zingeweza kuepukika kama sheria zingefuatwa.
No comments:
Post a Comment