Pages

KAPIPI TV

Monday, December 8, 2014

BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) TIMU YA MPIRA WA MIGUU SUNDERLAND (SAFC) ZATANGAZA UTALII WA TANZANIA UINGEREZA

1Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe na Garry Hutchinson Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya mpira ya Sunderland wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo kutoka kulia ni Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bw. Geofrey Meena, Teddy Mapunda mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya (TTB) na kutoka kushoto ni Mdau wa Utalii Bw. Nestor Mapunda na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshirikiana na Timu ya mpira wa miguu ya Sunderland (SAFC) ya nchini Uingereza katika uzinduzi wa utangazaji utalii wa Tanzania pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development). Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29 Novemba, 2014 kwenye kiwanja kinachomilikiwa na timu ya Sunderland “Stadium of Light”
(NA FULLSHANGWEBLOG HABARI NA MATUKIO ZAIDI YA PICHA SHUKA CHINI) 2Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi na kutoka kushoto ni Meneja wa Masoko wa (TTB) Bw. Geofrey Meena na Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Teddy Mapunda
 3 
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe na Garry Hutchinson Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya ligi kuu ya Uongereza ya Sunderland wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo huko Sunderland 04Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe katikati akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii kutoka kulia Meneja wa Masoko wa (TTB) Bw. Geofrey Meena, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi na kutoka kushoto ni Mdau wa Utalii Bw. Nesto Mapunda na Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Teddy Mapunda 4Wachezaji wa timu ya Sunderland wakipasha mwili huku wakiwa wamevalia fulana nyeusi zenye maandishi yanayotangaza na kukaribisha watalii na kutangaza utalii nchini Tanzania. 5Matangazo yakiendelea kuonyeshwa kwenye mbao za matangazo wakati mchezo kati ya Chealsea na Sunderland ukiendelea. 6Fulana zinazotangazo utalii wa Tanzania ikiwa zimewekwa kwenye vyumba vya kubadilishia jezi wachezaji wa timu ya Sunderland. 7Majarida yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamesambazwa kwenye meza katika mgahawa wa timu ya Sunderland kwenye uwanja wao wa Sunderland 8Mabango na yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamewekwa kwenye makumbusho ya timu hiyo. 9Haya ni baadhi ya mabango yanayoonyeshwa katika uwanja huo wakati wa michezo ya Ligi kuu. 10Bendera yenye maandishi ya kukaribisha watalii kutembelea Tanzania ikiwa imepandishwa katika miliongoti katika lango kuu la uwanja huo.

No comments: