Mratibu
wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akizungumza
jambo katika makabidhiano ya hundi kwa bwana Kennedy Kaupenda kushoto
kwake, Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii. Picha zote na Mpigapicha
Wetu.
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TAASISI
ya kifedha ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania,
imempatia Sh Milioni tatu mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu
kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya
Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.
Huduma hiyo mpya ya Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania ilianza mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya mzazi aliyejiunga na huduma hiyo kufariki Dunia.
Mwanafunzi
wa MUCE, Kennedy Kaupenda kushoto, akizungumza baada ya kukabidhiwa
hundi yake ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye Bima ya Elimu inayoendeshwa na
Bayport. Kulia kwake ni Mratibu wa Bima hiyo, Ruth Bura.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima ya Elimu inayotolewa na
Bayport Tanzania, Ruth Bura, alisema Kaupenda alitajwa kama mnufaika kwa
mzazi wake aliyefariki Dunia, hivyo waliamua kumtafuta kwa ajili ya
kumpatia mafao yake kwa ajili ya kuendelea kupata elimu bila vipingamizi
vyovyote.
Alisema
huduma hiyo ina vipengele vine ambavyo ni Bronze, Gold, Silver na
Exucutive, huku akisema kuwa makato ya kila mwezi ya Bronze ni Sh 2,500,
ambapo fao lake ni Sh Milioni 3, wakati makato ya Gold ni Sh 6,250,
huku fao lake likiwa ni Sh 7,500,000.
Ruth
Bura, Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania kulia akimkabidhi hundi
bwana Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu
baada ya kufariki mzazi wake.
Mratibu
wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura, kulia akizungumza
jambo baada ya kumkabidhi Kaupenda hundi ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye
huduma hiyo mpya iliyoanzishwa kwa ajili ya kukamilisha ndoto za elimu
kwa uwapendao.
“Pia
tunacho kipengele cha Silver ambapo makato yake kwa mwezi ni Sh 3,800,
huku mteja akilipwa fao la Sh Milioni 4,500,000 na kipengele cha
Executive kikihusisha makato ya Sh 9,000 na kumpatia mteja fao la Sh
10,800,000, huku tukiamini kuwa huduma hii ni sehemu ya kuhakikisha kuwa
Watanzania wanawawekea ulinzi wa elimu watoto wao na yoyote
wanayemchagua wao,” alisema Ruth.
Akizungumzia
fao hilo, Kaupenda alisema hakuwa na imani kuwa angesoma vizuri baada
ya baba yake kufariki, ila baada ya kutafutwa na Bayport na kutaarifiwa
juu ya mafao hayo, amepata nguvu mpya.
Kennedy
Kaupenda akitafakari baada ya kuiona hundi iliyoandaliwa kwa ajili yake
kutoka Bayport Tanzania juu ya fao la Bima ya Elimu.
“Nasikitika
sana baba kwa kunificha juu ya kujiunga na huduma hii sambamba na kuwa
mkopaji wa Bayport, hata hivyo namshukuru kwasababu fedha hizi zimekuja
kunipa mwanga mpya wa kuhakikisha kuwa nasoma kwa bidii, nikiamini kiasi
cha Sh Milioni tatu kitaniweka katika wakati mzuri mno,” alisema
Kaupenda, huku akiwasisitiza wazazi kujiunga kwenye huduma hiyo kwa
manufaa ya familia zao.
Mbali
na huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao, pia Bayport inajihusisha
na mikopo kwa watumishi wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, ambapo
mwishoni mwa mwaka 2014 walizindua huduma ya Mikopo ya Bidhaa, ambapo
bidhaa za bodaboda aina ya Lifan, Toyo na Boxer zinakopeshwa kwa wateja
wa Bayport Tanzania.
No comments:
Post a Comment