Pages

KAPIPI TV

Saturday, August 23, 2014

"BUZWAGI SI YA ZITTO" ASEMA KIGAILA


Na Magreth Magosso,Kigoma
 
WAKAZI wa Manispaa ya Ujiji Mkoa wa Kigoma waduwazwa  na Mkurugenzi wa Mipango na Mafunzo Taifa Benson Kigaila wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) kwa kitendo cha kumbeza ,Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini   Zitto Kabwe kwa kudai  skendo ya Buzwagi ni matunda ya uongozi wa juu wa chama hicho.
 
Kauli hiyo alitoa hapa hivi karibuni ambayo, iliwashangaza  wadau wa siasa  na baadhi yao kuzomea kauli hiyo na kudai  hiyo ni hila ya kutaka kumshusha thamani  aliyonayo mbunge huyo kwa jamii  husika ,ambao wanaamini  mbunge huyo ni shujaa na mtetea haki za wanyonge kwa kutanguliza utaifa badala ya  maslai ya chama .
 
Kigaila alisema  ukweli wa   hoja  alizotoa  Zitto  katika vikao mbalimbali vya  bunge ni mipango ya sekretarieti ambayo hukusanya taarifa zinazobainisha adha za wananchi na ili kufikisha ujumbe kwa serikali huwatumia wabunge wake, ili kupeleka kero  kwa wahusika kwa lengo la kustawisha jamii iliyopo.
 
Naye Katibu Taifa wa hapa Rafael Madede alipohojiwa na mwandishi wetu jana juu ya kutaka kufafanuliwa kuwa ni kweli hoja zitolewazo katika vikao vya bunge na wabunge hupikwa na uongozi wa juu wa  chama husika  akiri hilo na kudai  lipo wazi kwa waungwana  na kudai wananchi waliowengi hawana elimu sahihi ya mfumo wa vyama vya siasa na malengo yake.
 
“vyama vyote wanatumia mfumo wa kuibua hoja na kumpatia mbunge ili akawakilishe sehemu husika kwa maslai ya jamii zetu,changamoto wabunge wetu hujipa majina wao badala ya chama kilichoibua hoja husika  “ alibainisha Madede.
 
Jamii ikubali  wabunge wote hutoa  hoja kwa mlengo wa chama kulingana na uzito wa hoja ambayo ikifanyiwa maboresho ni tija kwa chama na jamii husika na kushauri  wananchi wawe na utaratibu wa kufuatilia midahalo na mikutano ya vyama ili kubaini uhalisia wa mambo na si kukubali mambo kwa utashi.
 
Pia  wananchi  wajifunze kikao cha ccm mkoani dodoma ,baada ya kikao hicho  walitoa  tamko  juu   rasimu  mpya ya katiba na ndivyo kwa  mbunge ni dhamana ya wananchi wenye haki ya kushika hoja kwa kuitetea katika vikao vya bunge  .
 
 Hivyo kazi ya kamati yoyote ile iwe Tasisi na Asasi za kiraia ni moja tu ambayo  hupanga na kuibua hoja na kumkabidhi mbunge  au diwani mwenye uelewa mpana , mvuto,utashi kwa jamii ili changamoto  husika iwawajibishe viongozi lengwa kwa chama tawala.

No comments: