Na Rose Masaka-MAELEZO_DAR ESALAAM
JESHI
la Polisi Kanda ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji watu
wanane kwa kutupa viungo vya binadamu katika bonde la Mbweni Mpiji eneo
la Bunju wilayani Kinondoni .
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaan Suleiman Kova amesema hayo
leo Ofisi kwake wakati wa mkutano na waandishi wa habari .
Amesema
kuwa watu hao wakimemo madaktari wa International Medical and
Technological University (IMTU) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi baada
ya kukiri kuhusika na tukio la utupaji wa viungo vya binadamu katika
eneo hilo.
Kamishna
Kova amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji na kufanya
uchunguzi kuona kama wahusika wamefanya kosa linalohitaji kuchukuliwa
hatua za kisheria au hawana kosa.
Ameongeza
kuwa kufuatia tukio hilo tayari Jeshi la Polisi Kanda Maalum
limeshafungua jarada la uchunguzi kubaini ikiwa wahusika wametenda kosa
linalohitaji kufikishwa kwenye vyombo vya sharia kwa hatua zaidi.
Kamishna
huyo amesema kuwa katika kutekeleza jambo hilo tayari jopo la
wachunguzi likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam Jaffar Mohamed linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha
watu hao kutupa viungo hivyo katika eneo hilo na idadi ya watu kulingana
na viungo vilivyotupwa
.
Aidha
Kamishna Kova amewasihi wananchi wasiwe na wasiwasi kwani viungo
vilivyookotwa havina uhusiano na mauaji ya watu wengi na wala
havihusiki na masuala ya ushirikina.
Amewaahidi wananchi kutoa taarifa kamili mara tu upepelezi utakapokamilika.
Viungo
vya binadamu vikiwemo mikono, miguu, vichwa , mapafu na mioyo
viligundulika jana (21.7.2014) jioni vikiwa vimehifadhiwa katika mifuko
ya plastiki 85 na kutupa katika bonde la Mbweni Mpiji eneo la Bunju
wilayani Kinondoni.
Mara
baada ya kugunduliwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni
walivichukua na kuvipeleka katika Hospitali ya Taifa kwa uchunguzi
zaidi.
No comments:
Post a Comment