Mtangazaji
wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akitia saini kitabu cha
wageni kwenye Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani.
Hapa akiwa mapokezi ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani huku akisema …Naipenda Tanzania yangu!
Hoyce Temu akiangalia baadhi ya picha za Mabalozi 15 ambao tayari
wameshaongoza Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani. wakiwemo Rais
Mstaafu Benjamin William Mkapa, Mustafa Nyang’anyi na Balozi Ombeni
Sefue pamoja Wanawake wawili ambao ni Mama Balozi Mwanaidi Maajar na
Balozi wa sasa Mh. Liberata MulaMula.
Mheshimiwa
Balozi Liberata MulaMula ndani ya mahojiano na mtangazaji wa kipindi
cha Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ofisini kwake jijini Washington DC,
Marekani!
Mahojiano
hayo ya moja kwa moja katika Balozi ya Tanzania nchini Marekani na
Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula ambapo wameangazia masuala
mbalimbali yakiwemo Utalii, kujitangaza katika miradi ya kimaendeleo na
uwekezaji ,malalamiko ya watanzania waishio Marekani kuhusu uraia, kwa
mengineyo mengi usikose kuangalia Channel Ten wiki ijayo Jumapili saa
moja na nusu usiku kilicho bora kabisa.
Na
wale waliokuja kuomba Visa wakapiga picha na aliyewahi kuwa mrembo wa
Tanzania na muongozaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu.
Hoyce Temu akipata picha ya ukumbusho na mpiga picha Iska JoJo aliyerekodi kipindi hicho.
Hoyce Temu anatoa shukrani za pekee kwa Blogger Mzee wa VIJIMAMBO DJ Luke Joe kufanikisha mahojiano ya Hoyce Temu na Balozi Liberata Mulamula.
No comments:
Post a Comment