Washindi
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka Kanda ya Ziwa
wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam
jana kwaajili ya Kuingia kambini tayari kwa safari ya kushindania
Milioni 50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane
Washindi
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kanda ya Nyanda za Kusini,
Stephen Mapunda(mwenye kofia nyekundu) na Mtawa Kaparata (mwenye fimbo)
wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere jana tayari kwa safari
ya kushindania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Washindi
wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini wakibadilishana Mawazo wakati
walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam
jana.
Washindi
wa Tanzania Movie Talents (TMT) wakielekea kwenye basi la TMT tayari
kwa kupelekwa kwenye Hoteli kwaajili ya Kupumzika mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam. Picha zote
na Josephat Lukaza
Na Josephat Lukaza – Proin Promotions Limited Dar Es Salaam.
Washindi
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka kanda zote za
Tanzania wamewasili jijini Dar Es Salaam jana kwaajili ya kuingia
kambini tayari kwa Kuanza safari ya kushindania kitita cha Shilingi
Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la TMT
itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Fainali
hiyo ya aina yake inayotarajiwa kutoa Mshindi mmoja mkubwa ambae
ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 ambapo washindi wengine tisa
wakiungana na mshindi mmoja watacheza filamu ya pamoja ambayo itauzwa
na kusambazwa na Kampuni ya Proin Promotions na washiriki hao kuweza
kunufaika na Mauzo ya filamu hiyo.
Mara
baada ya washindi 20 kutoka kanda zote sita wataingia Kambini mara
baada ya kutoka kupima afya zao na hatimaye mchakato wa kumpata mshindi
mmoja wa Shilingi Milioni 50 kuanza. Katika hatua hii ya kuanza
kumtafuta mshindi wa milioni 50, Majaji wa Shindano la Tanzania Movie
Talents (TMT) watakuwa wamepunguziwa majukumu kwa asilimia 40 na kazi
hiyo kuelekea kwa wananchi ambapo watawapigia kura washiriki ambao
wanawaona Wana vipaji na uwezo wa kuigiza.
Zoezi
hilo la Upigaji kura litaanza mara moja mara baada ya washindi hao
kuingia rasmi kambini na kuanza kupewa shule ya Sanaa na Walimu kutoka
Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo.
Wananchi watawapigia Kura kwa Kutuma Ujumbe Mfupi wa Maneno.
No comments:
Post a Comment