WANAUME wa Kata
ya Bangwe Mtaa wa Kamala mkoani hapa,wameandamana hadi kituo
cha Polisi kati kilichopo Manispaa ya Kigoma Ujiji,baada ya kuchoshwa na jirani
yao Joseph Peter (32) kwa kitendo chake cha kumpiga mkewe kila atokapo kupata
kilevi cha Pombe aina ya Kayoga.
Wakazi hao Sidney
Feles na Kasim Msenegal
kwa nyakati tofauti walisema ,Joseph anawapa
sifa mbaya wanaume
wenzake mtaani hapo,kutokana
na kitendo cha kumpiga mkewe mwenye
ujauzito mkubwa hadharani usiku kila
atokapo kunywa pombe.
Walisema kijana huyo anatumia fursa ya uyatima wa mkewe kumfanyia madhira hayo kutokana na
utegemezi wa kipato kwa mumewe hali inayomfanya avumilie kuishi kwenye dhiki na kipigo kutoka
kwa mwanaume huyo.
Naye Mhanga
wa kitendo hicho Anjelina Said (27) akiri kufanyiwa ukatili huo na mzazi
mwenzie Juni,13,2014 saa 5.00 usiku
aliporudi nyumbani hapo ambapo baada ya kufungua mlango na alipo ndani alianza kumpa kichapo hicho
kilichosababisha uso kuvimba.
“bado
nampenda japo sijafunga naye ndoa,ni mkorofi akinywa pombe,nina watoto wawili
na huyu kijacho atakuwa wa tatu,kwa kweli naumia ila ntafanyaje sina pa kwenda
,biashara sina nitaleaje watoto” alibainisha Mama huyo .
Kwa upande
wa Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Wilaya ya Kigoma Kaiza
alisema majirani wameandamana hadi hapa wakiomba akamatwe kijana
huyo,kutokana na kutumia ubabe wa nyadhifa
ya askari polisi jamii wa mtaa huo.
“sisis
tulifika pale saa 5.30 usiku nikiwa na vijana wangu alipotuona alitoa kauli
kali huku akishika panga lakini tulimsogelea na alipoona si majirani aliowazoea
ndipo akawa mpole na tumemlaza lupango hadi leo Juni ,17,2014 “
alibainisha Kaiza.
Kamishna Mwandamizi
wa Polisi wa hapa, (SACP) Frasser Kashai alisema matukio ya kupigwa
,kunyanyasika kwenye ndoa kina mama na watoto, kubakwa na kutelekezwa kimajukumu yamekuwa yakijitokeza kila wakati
kutokana na jamii kutoelewa athari za matukio hayo kwa sasa na siku za usoni.
Aidha
alionya wananchi kuwaonea huruma kwa kuwadhamini watu wanaofanya matukio ya
kikatili hali inayohamasisha miongoni mwa watenda wa vitendo vya ukatili kudharau sheria za nchi.
Baadhi ya wanaharakati
wa Asasi za kiraia zinazotetea haki za
kisheria watoto na wananwake kigoma Yasinta Ambrose( KIPACE) na Martha Jerome (WPC
) kwa nyakati tofauti wakiri wanawake wasijitambua ni wahanga wa vitendo vya
ukatili wa kijinsia hali inayochangiwa na utegemezi wa kipato.
Walisema wapo baadhi ya wanawake huingiliwa kinyume na
maumbile na waume na wapenzi wao kwa hofu ya kuogopa kuachwa ili walinde
heshima ya familia kwa kuogopa kuachika.Huku wakiwataka wananwake wabadilike
watumie,akili na viungo vya miili yao kutokana na hujuma wazofanyiwa na
wapendwa wao.
No comments:
Post a Comment