Mahmoud Ahmad Arusha
MAMLAKA ya mawasiliano nchini ,TCRA, imewaonya wale wote
wanaotumia mitando kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja
vinginevyo watakabiliwa na mkono wa sheria.
Onyo hilo limetolewa leo(jana) mjini Arusha na kaimu
mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRC, Dkt, Raynold
Mtungahema, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maswali ya wanahabari kuhusu
kuenea kwa picha chafu zinazowadharirisha watu mbalimbali kwenye
mitandao..
Mtungahema, amesema matumizi ya mitandao ambayo sio sahihi
ni kosa la jinai na hivyo wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja na
akawataka wanaochafuliwa kupitia mitandao wafungue majalada polisi na
mamlaka hiyo itasaidia kuwafuatilia wahusika na kuwafikisha mbele ya
vyombo vya sheria .
Alisema mitandao yote imesajiliwa hata kama aliyehusika
kuchafua anaishi uvunguni atakamatwa kwa kuwa mitandao haipo kwa ajili
ya matumizi yasiyo sahihi ambayo hayaruhusiwi.
Mtungahema, amesema atakaebainika anatumia mtandao
kumchafua mtu mwingine huyo amefanya kosa la jinai hivyo afikishwe mbele
ya vyombo vya sheria kwa kuwa tayari zipo sheria zinazotoa adhabu kwa
mtuhumiwa atakaepatikana na hatia.
Aliongeza kuwa TCRA, imeshapokea malalamiko mengi na tayari
wahusika wameshatiwa mbaloni na ufuatiliaji utaendelea ili mradi tu
mamlaka hiyo itaarifiwe .
Nchi wanachama wa jumuia afrika mashariki zimeaanza kikao
cha siku nne mjini Arusaha kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa chang moto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya mawasiliano.
Mwenyekiti wa jumuia hiyo ya sekta za mawasiliano, EACO,
Dakta Fracis Wangusi, amesema sekta ya mawasiliano inakabilwa na
changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha upatikanaji wa huduma za
mawasiliano kwa haraka.
Wangusi ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya
mawasiliano nchibni Kenya,amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na kuhama
kutoka mtandao wa analojia kwenda digital na matumizi ya visumbusi kwa
ajili ya luninga.
Aliongeza kuwa , sekta ya simu inakabiliwa na changamoto ya
kuwepo gharama kubwa za matumizi ya simu, usambazaji barua na vifurushi
kunakofanywa namashirika ya posta unaotokana na ukuaji wa mji ambao
haujapangiliwa ,matumizi ya vikwazo vya kuchelewesha huduma ya haraka
ya internet .
No comments:
Post a Comment