Na Magreth Magosso,Kigoma.
WAKAZI wa Kata ya Murungu wilayani
Kibondo Mkoa wa
Kigoma wamekuwa wakichapwa viboko kila wanapothubutu
kuchota maji katika chanzo cha maji
ya mto kumubanga kilichopo
ndani ya hifadhi ya muyowosi.
Akifafanua hilo Mwenyekiti wa CCM wa hapo Emanuel
Gwegenyezi alisema ,wananchi
wanaozunguka hifadhi hiyo wamekuwa na adha ya upatikanaji wa maji
katika eneo lao na kutegemea kisima kimoja tu ambacho
hakikidhi mahitaji ya kaya 6,000.
Alisema changamoto hiyo inawalazimu waingie ndani ya hifadhi
ya muyowozi na kuchota maji kwenye
chanzo cha mto Kumubanga ambapo wanakubwa na udhalili wa kuchapwa fimbo
na wahusika wa hifadhi kwa maslai ya kulinda chanzo hicho.
“adhabu ya kuchapa
fimbo waingiapo kuchota maji inachangiwa na msongamano wa foleni katika kisima cha kijiji,mama akienda asubuhi saa 12
atarudi saa 1.00 jioni,kiuchumi
jamii haizalishi”alibainisha
Gwegenyezi.
Mkuu wa wilaya hiyo Venance Mwamoto akiri kuwepo kwa adha ya maji kwa wakazi
hao,lakini apata mashaka kupewa uhuru wa kuchota maji masaa 24,kutokana na kijiji hicho kukithiri kwa matukio ya upatikanaji wa silaha za moto.
“ mwaka jana tulipata silaha hizo si chini ya 270 kutoka kwa
wakazi wa hapo, si wote kwa ajili ya maji ,wapo wajanja wanaokwenda kupata
upenyo wa kuingia hifadhini na kufanya mauwaji ya wanyama” alibainisha Mwamoto.
Alisema mwenyekiti wa kijiji,diwani hawana uchungu wa
kushughulikia adha za raia wao,kutokana na kushindwa kutatua adha hiyo kwa
kuishirikisha idara ya maji na mwekezaji kutumia mto huo kuvuta maji kwa pampu
na kuwajengea kisima chenye kukidhi hitaji hilo.
Katibu mwenezi Mkoa Kalembe
Masoud na mwenyekiti wa ccm wilaya Kassim Kasambwe kwa nyakati
tofauti walisema vijiji vilivyopakana na
mapori ya hifadhi mkoani hapa yanakabiliwa
na changamoto ya ukosefu wa amani hali inayozidi kuchochea chuki baina ya mwekezaji na umma husika.
Baadhi ya wananchi
waishio karibu na hifadhi hiyo Jonathan Joel na Mwamila Madirisha kwa nyakati tofauti walisema serikali hutoa
ardhi kwa wawekezaji pasipo kuweka mfumo
wa kumbana mwekezaji iheshimu haki za jamii husika.
Akijibu tuhuma hizo, meneja wa hifadhi hiyo Mathias Ngasila
alisema, changamoto hizo zipo nje ya uwezo wake kwa mujibu wa sheria na sera ya
hifadhi za mapori na kuahidi Agosti,2014
atafanya mkutano na jamii husika kutatua migogoro inayohusu hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment