Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete leo amemwapisha balozi mmoja pamoja na wajumbe wanne wa
Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini
Dar es Salaam leo mchana.Balozi aliyeapishwa ni Joseph Edward
Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Wajumbe walioapishwa nia
pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi,Jaji
Mstaafu Steven Ernest Ihema,Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo pamoja na
katibu wa tume hiyo Bwana Frederick Kapela.



No comments:
Post a Comment