Na Mwandishi wetu, Zanzibar
NGALAWA
zote 11 zilizoingia majini kukamilisha mzunguko wa saa mbili wa resi za
ngalawa mjini Zanzibar zilimarisha mashamshamu hayo bila najali na timu
tatu zilipewa zawadi za ushindi.
Resi
za Ngalawa kama zinavyojulikana ni utamaduni halisi wa visiwa vya pemba
na Unguja na ni sehemu ya tamasha kubwa la filamu la kimataifa la
Zanzibar ambalo linaendelea visiwani hapa.
Kwa
wale waliozaliwa maeneo ya bara, resi hizi zilikuwa kivutio kikubwa kwao
kutokana na maandalizi yanayofanywa kabla ya kuingia majini na dau
kunyanuliwa.
Wakati
dau limenyanyuliwa, maji yamekuwa yakichotwa ama ndani ya Ngalawa au
nje katika bahari kumwagia tanga katika hali inayoelezwa kuliimarisha
katika ukinzani wa upepo.
“mbio
za Ngalawa ni kipimo kikubwa cha Uzanzibari wetu na kila mwaka ZIFF
huhitimisha utashi wake wa kuwa na tamasha la nchi za jahazi kwa kuwa na
mbio za ngalawa” alisema mshehereshaji Muslim Nassoro Abdalla katika
shamrashamra zilizofanyika ufukweni kandoani mwa hoteli ya Tembo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe.
Mahmoud Thabit Kombo (mwenye t-shirt ya njano) akupiliza Kipenga
kuashiria kuanza kwa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye fukwe za
Hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.
Muslim
ambaye alisema kwamba mwaka huu walitaka kuwa na mbio za timu 20
(ngalawa) walishindwa kuhitimisha ndoto hiyo kutokana na masuala nje ya
uwezo wa ZIFF.
Ili kukamilisha vyema mbio hizo kunatakiwa kuwa na boti za kutosha za uokozi kama kutatokea ajali.
Mwaka
juzi kulitokea ajali ambayo hata boti ilipofanya uokozi nayo ikazidiwa
na kulazimisha watu kukwama mpaka jioni walipopata boti nyingine kutoka
Bandarini.
Wakati
wa mbio za resi ambazo washindi wa kwanza ni timu iliyokuwa ikiongozwa
na Hatibu Suleiman waliokuwa ndani ya ngalawa Ipo Siku, ngoma mbalimbali
za asili zilipigwa ufukoni kama hamasa huku watu wakisubiri marejeo ya
ngalawa hizo.
Baadhi ya Ngalawa zinazoshiriki mashindano hayo zikianza kukata mawimbi.
Mbio
hizo ambazo zilianzishwa na mbunge wa Kiembesamaki na Mwenyekiti wa Bodi
ya ZIFF, Mahmoud Thabiti Kombo mshindi wake wa pili alikuwa ni timu ya
haji Hassan (kama nadhodha) ndani ya ngalawa Kipanga. Aidha Hassan Simai
na wenzake waliokuwa katika ngalawa iliyoitwa peace of Love walikuwa
washindi wa tatu.
Timu
ya ngalawa ambayo inahitaji ujuzi katika utekaji tanga , kulirekebisha
na kubalansi ngalawa inahitaji watu wapatao watano na si chini ya
watatu.
Tamasha
la filamu linaendelea mjini hapa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za
mafunzo ya utunzi, utengenezaji wa filamu na uhakiki wake.
Pichani juu na chini ni Sehemu ya wakazi wa Zanzibar wakishuhudia mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment