Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam waliojitokeza katika zoezi la uchangiaji wa damu kwa hiari wakipata maelekezo kutoka kwa Meneja wa Huduma za Kitabibu wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Tanzania Bw. Rogation Selengia ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya uchangiaji ya kuchangia damu duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Damu salama kwa ukombozi wa wanawake”zoezi hilo liliendeshwa mwishoni mwa wiki kwa ushirikiano wa Mpango wa Taifa wa damu salama na Kampuni hiyoPICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Tanzania Bw. David Ludovick (kushoto) akitoa maelezo ya kina kwa mmoja wa wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo. uchangiaji damu kwa hiari katika kilele cha siku ya uchangiaji damu duniani,lilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mlimani City jijini. Mmoja wa wauguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu salama akimpima mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, aliyejitokeza katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari. Ofisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Bi. Selina Sahani akimtoa damu Meneja Mauzo wa kampuni ya Bima ya Jubilee Tanzania Bw. David Ludovick. Baadhi ya wahudumu kutoka Mpango wa Taifa wa damu salama wakitoa maelekezo na upimaji wa wingi wa damu kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu.
No comments:
Post a Comment