| Mama Salma Kikwete akiwa na kikundi cha ngoma ya asili inayofahamika kwa jina la Mapigo tisa mkoani Kigoma wakati wa Maadhimisho ya Uchangiaji damu. |
Na Magreth
Magosso,Kigoma
Akifafanua
hilo kwenye kilele cha uchangiaji wa Damu salama ambapo kitaifa ilifanyika
mkoani hapa, katika
uwanja wa Lake Tanganyika ambapo
pia alikuwa Mgeni rasmi katika kilele hicho alisema,
watumishi wasio na maadili mema ni chanzo cha jamii kusuasua kushiriki katika suala la uchangiaji Damu salama.
“wananchi,
shirikianeni kuwaumbua watumishi wasio na madili ,wanaotumia fursa ya wahanga
ili wajipatie kipato haramu,damu haiuzwi na mkigundua mtumishi wa hivyo jamani
mfichueni ili apate haki yake” alibainisha Mama Salma.
Pia alisema
wananchi waliowengi wanaogopa kujitokeza
kuchangia damu kwa hofu ya kukutwa na maradhi mbalimbali ya mambukizo kitendo ambacho kinachangia
wananchi kuishi maisha mafupi ,kutokana na kuishi na maradhi ambapo
wakibadilika kwenda kupima kila wakati ni rahisi kupata tiba ya ugonjwa husika
.
Kwa upande
wa Mkurugenzi wa Evidence For Action Craig Ferla alisema asasi za kiraia na
serikali walipe uzito changamoto ya vifo vya kinamama wajawazito ambapo kina mama 8,000 hupoteza maisha kila
mwaka wakati wa kujifungua kutokana na
kutokwa na damu nyingi ambao unachangiwa na ukosefu wa damu ya akiba kwa ajili ya kuepusha vifo
hivyo.
Alisema Kigoma
imeonyesha njia ya kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa kufanikisha lengo la kimkoa katika uchangiaji damu,ambapo chupa 3620 zimepatika katika wilaya sita
mkoani humo, licha ya mkoa huo kutakiwa kutoa chupa 3000 za damu hiyo.
Naye
Mwakilishi wa Tasisi ya CDC Dr.Regina Kutaga alisema changamoto ya ukosefu wa damu salama katika benki ya damu katika
sekta ya afya inachangia vifo vya uzazi kwa 80% sanjari na kukwamisha
malengo husika kuwa, ifikapo 2020 kila
nchi ifanikishe kuwa na damu salama kwa 100%.
Kwa upande wa Meneja wa Damu salama Taifa Dr.Abdul Juma na
Meneja Damu salama kanda Magharibi Ipyan Kaganuka kwa nyakati tofauti walisema wameanzisha mfumo rasmi wa kuweka kumbukumbu za majina ya wathubutu wa uchangiaji damu ambapo itasaidia kupata idadi ya uchangiaji wao sanjari na
kupatiwa motisha.
Walisema
lengo ni kuwawekea utaratibu wa uchangiaji
wao wa kuchangia damu salama kila
ifikapo wakati wa kufanya hivyo.huku wakiri kufikia lengo la kitaifa ambapo zilihitajika
chupa 6500, ambapo jana katika sherehe za kilele cha shughuli hizo walipata chupa 7,000 ambazo bado
hazijakaguliwa kitaalamu zaidi kama zipo salama.


No comments:
Post a Comment