Na Magreth Magosso,Kigoma.
Wajawazito
wanaolazwa katika hospitali ya Ujiji wamepunguziwa adha ya kutumia khanga kutandika vitanda vyao, pindi walazwapo katika hospitali hiyo, baada
ya kituo hicho kukabidhiwa mashuka 100, kutoka Mfuko wa Taifa Bima ya Afya kwa lengo la kuboresha afya ya mama na mtoto.
Akikabidhi mashuka hayo
hospitalini hapo Ally Mchumo
ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya mfuko huo(NHIF) alisema msaada huo umelenga madhimisho ya
siku ya wadau wa mfuko huo ambao hufanyika kila mwaka ,hawana budi kutumia fursa hiyo kama sehemu ya mchango wao kwa
jamii husika.
Balozi
Mchumo alisema kiasi cha sh.milioni 294 zimetumika katika mashuka hayo
ambayo ni tija kwa wadau ,Huku akiwataka wakuu wa idara ya afya watumie
fursa ya huduma ya Mikopo ya
ghalama nafuu ya mfuko huo ili kusaidia kupunguza adha ya vifaa tiba .
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo John Magiga
alisema wadau wa afya wanawajibu
wa kutambua adha na kupunguza changamoto katika vituo vya afya, zahanati katika mikoa iliyopo pembezoni
mwa nchi ambayo ipo nyuma kimaendeleo.
Baadhi ya wagonjwa
Latifa Omari na Neema Joshua kwa nyakati tofauti walisema wajawazito wamekuwa
wakitumia khanga kutandika vitanda,kutokana na uhaba wa mashuka hivyo kuwa na
wakati mgumu wakati wa kujifungua kwa wale wasio na nguo za kutosha .
Naye Muguzi wa kituo hicho
Siwazuri Mwinyiomvua amekiri msaada huo utapunguza adha hiyo,ambapo ilikuwa ikiwathiri
kisaikolojia wajawazito walio na kipato
cha chini hasa wanapokosa mashuka ya kutandika vitanda .
Muuguzi Mkuu wa Wilaya hiyo Joyce Malekela alisema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa maji,watumishi pamoja na vitendea
kazi hali inayowalazimu watumishi kufanya kazi katika mazingira magumu.
Naye Meneja Mfuko (NHIF) Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo aliwataka viongozi
wa Mkoa huo na wanasiasa waongeze
uhamasishaji kwa jamii wajiunge
na mifuko ya afya NHIF na CHF ili waondokane
na gharama kubwa za matibabu ya papo kwa papo.
Aidha
mfuko
unalenga kutoa huduma kwa wakazi wote ambapo kwa mwaka 2013 mfuko
umefikia
asilimia 15% ya wanachama kwa Mkoa wa Kigoma na wanatarajia wanachama
waongezeka kwa 30% ,kama kauli mbiu ya serikali inavyotaka umma ujiunge
na mfuko huo.




No comments:
Post a Comment