Pages

KAPIPI TV

Thursday, May 22, 2014

KASHAI AKATAA FEDHA ZA NRA-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma
IMEFAHAMIKA kuwa,Kamanda  Mwandamizi msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kigoma,Frasser Kashai amedaiwa kukataa kupokea  kiasi cha Shilingi laki moja  kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa choo cha askari polisi kituo cha Mwandiga, zilizotolewa na  Chama cha NRA  kigoma .

Akifafanua tukio hilo katibu wa chama hicho Rashid Tanganyika alisema awali waligundua changamoto ya ukosefu wa choo kwenye ziara ya katibu wa Taifa NRA 2012-2013 alipotembelea idara mbalimbali  wilayani  kigoma na kubaini kituo cha polisi cha mwandiga hakina choo zaidi ya miongo kumi. ,hali inayowafanya askari husika kujisaidia kwenye vyoo vya wananchi.

Alisema  kutokana na mazingira hayo tete ,katibu Taifa wa chama hicho Hamis Kiswaga aliahidi kwa RCO wa hapa Dismas  Kisusi kuwa atachangia fedha hiyo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha  idara ya polisi ikamilishe ujenzi wa choo cha mwandiga ili kulinda heshima na hadhi ya walengwa.

Naye Katibu Taifa wa chama hicho Kiswaga alisema alitoa fedha hizo ,baada ya kubaini baadhi ya wananchi kuwashusha thamani askari wa kituo hicho ambapo inachangia  askari husika  kutowajibika kikamilifu ,kutokana na baadhi ya washukiwa wa uhalifu  wanawasaidia kujisitiri kwenye vyoo vyao.

Alidai  kitendo cha Kamanda huyo, kukataa kupokea fedha hizo ni udhaifu wa uwajibikaji kwa jamii na kupelekea wadau wengine washindwe kusaidia idara hiyo na kushauri aweke mpango mkakati  wa kuondoa dhana hasi penye changamoto .


Akijibu shutuma hiyo Kamanda Frassser Kashai  amekiri kukataa kupokea kwa sababu ya  gharama kubwa ya lengo husika,hivyo amehofu  fedha hiyo kutumika sivyo ndivyo kutokana na changaoto ya fedha za ziada katika  ujenzi wa choo hicho.

Alisema endapo angepokea fedha hizo na kutokamilika kwa ujenzi huo 2013 ,angesemwa kwenye jukwaa la wanasiasa huku akimpa jukumu hilo OCD Medrad Singano afanyie tathimini wa ujenzi huo na atoe mrejesho wa tathimini kwa wadau ili kuondoa dhana ya kukataa kwakwe  .

Baadhi ya wananchi walipohojiwa dhana ya usafi na magonjwa ya mlipuko Mariam Issa na Judith Emmanuel kwa nyakati tofauti walisema , serikali inahamasisha umma namna ya kusafisha mazingira hasa usafi wa nyumba na vyoo  bora  ili  kuepukana na magonjwa ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa Dengue.

Gazeti hili limebaini  Jeshi la polisi la hapa lipo njia panda kubuni njia mbadala wa kuhakikisha vituo vyake vina vyoo  bora na vya kisasa ,ambapo  mbali ya kituo cha Mwandiga pia changamoto hiyo ipo kituo cha polisi cha Ujiji kutokana na choo chake kujaa kinyesi na askari husika kujisaidia vivyo hivyo.

No comments: