Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 21, 2014

ASKARI FEKI WA JWTZ ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI TABORA


Kamanda wa Polisi ACP Suzan Kaganda akionesha sare za Jeshi la Wananchi JWTZ kwa waandishi wa habari  zinazodaiwa kutumiwa kimakosa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Karimu Ally akidai kuwa ni askari wa JWTZ,hufanya hivyo kwa kutaka kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 19/05/2014.

Ndugu waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linaendelea na Operesheni katika wilaya zote za mkoa wa Tabora. Ambapo kufuatia operesheni hiyo tumefanikiwa kukamata watuhumiwa wa makosa  mbali mbali kama ifuatavyo:-

KUPATIKANA NA RISASI: Mnamo tarehe 18/05/2014 huko eneo la barabara ya Sikonge kata ya Ng’ambo Manispaa ya Tabora alikamatwa BARANABA s/o JOSEPH, 36yrs, Mkonongo, mkazi wa Inyonga wilaya ya Mlele  mkoa a Katavi akiwa na risasi 307 za SMG/SAR, mtuhumiwa amekiri kujihusisha uchuuzi wa risasi na matukio mbalimbali ya unyanga’anyi wa kutumia silaha. Baada ya mahojiano alieleza kuwa risasi hizo ameuziwa na CHRISTINA D/O PILIPILI, 42YRS, muha, mkazi wa mataa wa Hali ya hewa, kigoma mjini ambaye naye amekiri kuwa ni muuzaji wa risasi na huzitoa maeneo ya kigoma na kuja kuuzia hapa mkoani Tabora na mikoa mingine ya jirani . Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada baada ya upelelezi kukamilika.


KUPATIKANA NA SARE ZA JESHI: 
tarehe 18/05/2014 huko eneo la Isike jirani na NBC Bank manispaa ya Tabora alikamatwa KARIMU S/O ALLY, 25yrs, Muhurudu mkazi wa Mirambo, akiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Mtuhumiwa amekuwa akitishia na -kulaghai wanachi kuwa ni askari wa jeshi hilo kwa nia ya kujipatia fedha na huduma mbalimbali. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.


KUPATIKANA NA SILAHA: 
katika eneo la Ndono wilaya ya Uyui alikamatwa, RAJABU S/O HUSSEIN, 65yrs, Mnyamwezi, mkulima mkazi wa Kidatu manispaa ya Tabora akiwa na silaha aina ya Shortgun iliyotengenezwa kienyeji kinyume na sheria, kisu kimoja kikiwa ndani ya ala, tochi moja na Risasi tatu za Short gun. Mtuhumiwa baada ya kukamatwa aliwataja watu wawili wanaomuuzia risasi ambao ni:- NOEL S/O VITALI, 40yrs, mkulima, na ADREA S/O JOSEPH, 50yrs, Mnyamwezi, wote ni wakazi wa Ukumbisiganga wilaya ya Kaliua, wameshakamatwa tarehe 15/05/2014.upelelezi unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani.


Pia huko eneo la usoke mjini kata na Tarafa ya usoke wilaya ya urambo walikamatwa HIRALY S/O RASHIDI @ BAKARI 40YRS ABDALAH S/O RASHID @BAKARI 35YRS, MOSHI S/O RASHID @BAKARI 38YRS NA ALADIN S/O RASHIDI @BAKARI 22YRS wote wakazi wa Usoke mjini wakiwa na bunduki aina ya RIFFLE na risasi tano ambayo wanamiliki kinyume na sheria. Upelelezi unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani.


AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO: 
huko kijiji cha Bulyang’ombe barabara kuu ya Igunga –Nzega gari lenye namba za usajili T.677 AGJ Scania bus mali ya ZUGA s/o AUGOSTINO @RICHARD wa Mwanza ikiendeshwa na PIUS s/o? iligonga gari T.968 AJX Iveco iliyokuwa imeegeshwa pembeni mwa barabara na dereva JUMA s/o BUNDALA, 41yrs, msukuma, mkazi wa Shinyanga na kusababisha vifo vya watu 2 na majeruhiwa 14 wamelazwa katika hospitali ya (w) Igunga . chanzo ni uzembe wa dereva.


Jeshi la Polisi (M) Tabora linatoa shukurani kwa wote wanaolipatia taaarifa tunazidi wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi lao ili kukomesha na kutokomeza vitendo vyote vya uhalifu na kuwafichua wahalifu, pia  watumiaji wa barabara wafuate  sheria za usalama barabarani ili kupunguza matukio ya ajali  Operesheni za kukamata wahalifu na makosaya baarabarani zinaendelea ili kuhakikisha mkoa unakuwa na amani,utulivu na usalama wa raia na mali zao.

Imetolewa na :-

KAMANDA WA POLISI

MKOA WA TABORA.

No comments: