WANAKIJI 15
katika Kijiji cha Chagu Kata ya Mtego wa noti Wilaya ya Uvinza
Mkoa wa Kigoma wamekufa baada ya kuliwa na Mamba waliopo kwenye bwawa
la Mngonya kwenye eneo la kilomo.
Kitendo
hicho kinaathiri shughuli za uvuvi sanjari
na kupungua kwa nguvu kazi ya kijiji hicho huku watendaji na viongozi wa idara
husika wamefumbia macho suala hilo ili
hali watu wanakufa hali iliyochangia wananchi
wapeleke kilio chao kwa Mwenyekiti wa Chama cha CCM mkoa Dr.Warid Kaburu atoe kauli ya utendaji kwa
watendaji na wahusika kuondoa adha hiyo.
Baadhi ya
wanakiji Resdey Gasper na Rahel Mbogota
kwa nyakati tofauti walisema vijana wao wanaangamia pindi waendapo kuvua samaki kwenye bwawa hilo,kutokana na
mamba kuongezeka kuzaliana kila mwaka sanjari na kuongezeka kwa vifo vya watoto
wao kuliwa na wanyama hao ambao hawaoni faida ya
kuendelea kulindwa na idara husika.
Akijibia
hilo Mwenyekiti wa chama cha CCM Dr.Warid Kaburu amekiri mapungufu ya utendaji
wa kazi kwa wahusika katika hilo hali
inayochangiwa na watendaji wa kijiji kwa kushindwa kuweka mkakati mahususi wa
kuondoa janga hilo.
“sioni
sababu ya wahusika kushindwa kuwaua mamba ambao wametafuna watu 15 ajabu wapo
kimya hii inatafsiri liachwe kwa faida ipi ya mapato juu ya mamba wala
watu,jamani hili wahusika wachukue hatua “ alisema Dr.Kaburu.
Awali katika
mkutano huo Diwani wa kata husika Sindano Selukala aliwataka wakazi wake watoe
changamoto zenye mashiko ili seriakali iwajibe kwa mujibu wa sera,kanuni na
taratibu za utawala bora kwa lengo la ustawishaji wa jamii husika ili waishi
kwa amani .
No comments:
Post a Comment