Pages

KAPIPI TV

Monday, April 28, 2014

WANAKIJIJI KAZULAMIMBA WALILIA ARDHI -KIGOMA

 
Na Magreth Magosso,Kigoma

Wananchi  wa Kijiji cha  Kazulamimba wilaya ya uvinza Mkoani hapa,wameitaka serikali itazame upya kuwaongeza eneo la kilimo kwenye kijiji hicho ,kutokana na idadi kubwa ya wakazi kuongezeka.

Pia kijiji kimeathiriwa na kupakana  na pori la hifadhi ya Nyabikoke  ambapo wakazi 3,750 kitongoji cha kidea baadhi ya wakulima wameacha kulima kwa kile kinachodaiwa kufukuzwa na wamiliki wa maeneo hayo waliomilikishwa mwaka 1990.

Akifafanua hilo Mwenyekiti wa chama cha NRA wilayani hapo  Maulid Gwimo  alisema zahanati na shule ya msingi  kazulamimba ,imo ndani ya hifadhi ya nyabikoke,hali inayowachanganya wananchi kutoelewa mipaka yao halisi kisheria na taratibu za misitu.

Alisema akiwa mmoja wa mjumbe wa baraza la Ardhi kijiji hicho wamepokea mashauri 20 juu ya migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji na baina ya mmiliki wa shamba na waliovamia maeneo kutokana na baadhi ya wamiliki kushindwa kuyaendeleza mashamba hayo.

Baadhi ya wanakijiji  Hussein Manta ,Japhet na Yozephina Ndikumwenayo kwa nyakati tofauti walisema hali ya kukosa maeneo ya kulima imekuwa ni kigezo cha vijana kushinda vijiweni na mimba za utotoni kwa vijana wa jinsi ya kike.

Walisema upembuzi yakinifu unahitajika kubaini mapungufu yaliyopo katika sheria ya misitu ili kukidhi hitaji la wakazi kwa mujibu wa takwimu ya leo na si takwimu ya wakazi ya miaka ya nyumba ambapo kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji vya ujamaa.

Kwa upande wa Katibu Taifa chama cha NRA Hamis Kiswaga na Katibu Mkoa Ramadhan Tanganyika kwa nyakati tofauti walisema,serikali iweke mpango wa kugawa mashamba yaliyotelekezwa sanjari na hati miliki kwa mashamba telekezwa kwa sheria husika.

Mwenyekiti wa Chama cha CCM Dkt.Warid Kaburu alisema ili migogoro ya ardhi iishe serikali  ifanye maamuzi ya busara kuboresha sheria ya misitu kwa lengo la ustawishi wa jamii kwa maslai ya kudumisha utulivu uliopo nchini.

Diwani  wa kijiji hicho Kassian Mabondo akiri baadhi ya wamiliki  wakubwa wa mashamba katika kitongoji cha kidea kata ya kazulamimba wametelekeza maeneo kwa muda mrefu hatimaye jamii imeyahozi kwa kilimo ambapo sasa wamiliki wa awali wanadai maeneo yao.

Mkuu wa wilaya hiyo Hadija Nyembo alipohojiwa juu kadhia ya wakulima kuacha kulima kutokana na kukosa ardhi eneo la  kidea alisema hajui huku mwenyekiti wa kijiji hicho Feles Buyaga awasihi wananchi wapeleke malalamiko ngazi husika.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 1994 kulikuwa na wakazi 200 sanjari na shule moja ya msingi iliyoitwa `kazulamimba’na  leo 2014  kuna shule saba ambapo  shule  moja ni ya sekondari .

No comments: