Na Magreth Magosso,Kigoma
Jambazi
mmoja aliyevaa sare za jeshi ya nchi ya Burundi auawa na askari wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma
katika harakati za kurushiana Risasi na
askari hao.
Hali hiyo imekuja baada ya
majambazi watatu waliovaa sare ya nchi hiyo(Burundi) walimteka mwalimu wa shule
ya msingi Minyima nyumbani kwake na kupora fedha taslim sh.200,000 sanjari na
simu aina ya tekno,ndipo askari walifanikiwa kupata taarifa na kuanza msako mkali na
kufanikiwa kuwaona kwenye kichaka na kuanza kurushiana risasi na jambazi huku mmoja
akifariki dunia papohapo.
Akithibitisha hilo Kamanda
wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Fraizer Kashai alisema majira ya saa 2.30 usiku, Aprili 22,
2014,katika pori la Samvura kata ya Bunyambo Wilaya ya Kibondo majambazi watatu
wakiwa na Silaha aina ya SMG moja na Magazine
walimteka mwalimu Engliberth Robert(34)
Alisema jambazi hilo akiwa
na wenzake walifanikiwa kudhibitiwa na askari Polisi wa kituo kidogo cha
Bunyambo na kufanikiwa kufanya msako ambapo walimuua jambazi mmoja kwa risasi.
Pia katika tukio hilo askari
walifanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG No. 196XN9897 na Risasi 43 ambazo
walikuwanazo majambazi hayo,huku akiwapongeza askari husika kwa kudhibiti tukio hilo.
Na mwili wa jambazi huyo upo
hospitali ya wilaya ya kibondo kutokana na
kutotambulika na majambazi wengine wawili walifanikiwa kukimbia hivyo
juhudi za kuwasaka zinaendelea.
Katika tukio lingine mtu
mmoja ambaye hajafahamika aliwapigia simu polisi na kuwaelekeza sehemu aliyoona
silaha aina ya SMG yenye no. 1952 GAW 2882 ikiwa na magazine moja yenye risasi
23 za SMG kwenye mfuko wa salfeti.
No comments:
Post a Comment