Pages

KAPIPI TV

Tuesday, April 22, 2014

MTOTO APOTEZA MAISHA KWA KUANGUKIWA NA UKUTA KANISANI SIKU YA PASAKA-KASULU

Na Magreth Magosso,Kigoma
Mtoto mmoja (05)Adela Kambi anayesoma  shule ya awali  katika  kambi ya wakimbizi Nyarugusu  wilaya  ya Kasulu  mkoani  hapa   amekufa baada ya kuangukiwa na ukuta wa kanisa la Full Pentekostal churches Tanzania(FPCT) siku ya sikukuu ya Paska.

Akielezea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa huo,Frasser Kashai alisema,April,20,2014  saa 3.30 katika kanisa hilo ambalo lipo kambini hapo,lilianguka muda mfupi baada ya kumaliza ibada ya sikukuu ya pasaka na kupelekea kifo cha mtoto huyo.

Kamanda huyo alibainisha chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa jengo hilo chakavu likichangiwa na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo kusababisha matofali kuanguka na kusababisha kifo hicho  na kujeruhi wakimbizi wengine wawili.

“waliojeruhiwa na ukuta huo ni pamoja naGedion Bigira(42) alivunjika mguu wa kushoto na ,Omari Selestine(30) pia alivunjika mguu wakushoto na wapo hospitali ya kasulu wanatibiwa majeraha hayo” alidai kamanda huyo.
 
Aidha katika tukio la pili zaidi ya wahamiaji haramu 125 mkoani hapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kitendo chao cha kuingia nchini kinyemela.
Kamanda Kashai alisema kutokana na msako wa doria endelevu unaofanywa na polisi katika wiki mya sikukuu ya pasaka askari polisi wamefanikiwa kukamata wahamiaji hao sanjari na kete 260 za mihadarati sambamba na lita 240 za pombe haramu aina ya gongo.

No comments: