Pages

KAPIPI TV

Thursday, April 10, 2014

MARUFUKU BODA BODA NA BAJAJI ZA ABIRIA KUVUKA MWENGE KWENDA POSTA


boda 1
Oparesheni Kamata Bodaboda na Bajaji ikiwa inaendelea upande wa Mwenge mataa ambapo Bajaji nyingi zimekamatwa.
IMG_0003
Askari wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha Polisi.
IMG_0010
Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa.
IMG_0012
IMG_0018
Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimekamatwa.
IMG_0020
  Madereva wa Boda Boda na Bajaji wakipata maelezo ya kina ya kwanini wamezuiliwa  kwenda Posta wakitokea Mwenge.
IMG_0021
Mmoja wa Madereva wa Bodaboda akiwa amekaa kwa mawazo asijue anafanya nini Baada ya Bodaboda yake kukamatwa na Kupelekwa Polisi.(Picha na Dar es salaam yetu).


Kwa mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.

“Tumefanya hivi ili kuepusha msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili kupunguza tatizo hili. 

Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo”Hiace” pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa”  alimalizia kwa kusema “Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali” alisema Polisi huyo.
Kwa mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda maeneo hayo.
Wanao ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.

No comments: