Pages

KAPIPI TV

Monday, March 3, 2014

KIGOMA HATARINI KWA UGONJWA WA AKILI

Na Magreth Magosso,Kigoma

Zaidi ya  wastani wa Wananchi 777  waishio Mkoa wa Kigoma wapo hatarini kupata ugonjwa wa akili unaochangiwa na utumiaji wa dawa za kulevya sanjari na ugumu wa maisha.

Akifafanua kauli hiyo,Kigoma ujiji kwenye kikao cha utoaji takwimu juu utambuzi wa afya kwa wagonjwa wa akili,(TUSPO)  Kaimu Ofisa Uchumi wa Manispaa ya Kigoma ujiji  Bw.Kalila King alisema  utafiti uliofanywa na asasi hiyo inabainisha kuwa kata ya Gungu ina wagonjwa wa akili wapatao 91 ambao wameathirika na dawa haramu za kulevya  pamoja na msongo wa mawazo.

“ Kigoma ina zaidi ya wakazi laki mbili na kwa kata hii ina kaya 94  ina maana kila kaya ina mgonjwa wa akili  mmoja kwa mujibu wa tafiti na  hapo bado kata ya  Ujiji ambapo watumiaji wapo wazi hali ni mbaya wahusika tuwajibike” alidai King.

Kwa upande wa Katibu wa asasi hiyo Bw. Elias Lukata alisema uwepo wa wathirika wa akili upo kata ya Gungu ambapo katika mitaa minne waliyofanya utafiti wamegundua wagonjwa wa akili  91 ambao wamegawanyika  katika makundi 3 wakiwemo waliozaliwa nao wapo 7,  dawa za kulevya unga wapo 46,wakati wavuta bangi wamepatikana 29 huku wale wanaosumbuliwa na  msongo wa mawazo hata kufikia hatua ya kuathirika na kupata magonjwa ya akili walipatikana  9.

Alisema hali hiyo inachangiwa na ukosefu wa ajira na hata pale viongozi wa Manispaa  ya Kigoma kutokuwa na kipaumbele cha vijana kupitia fungu lao la fedha kwa mujibu wa sera ya nchi hali inayowakwaza na kushindwa kufikia ndoto zao kupitia fursa hiyo.

Kwan upande wa mgeni rasmi kwa niaba ya katibu tawala Manispaa ya Kigoma Bw. Rashid Maftaha alisema ni vyema asasi hiyo ikashirikisha halmashauri katika vipaumbele vya bajeti ili watengewe fungu la kuweza kufanya tafiti katika kata zilizobaki  mkoani humo hatua ambayo itaweka wazi ukubwa wa tatizo hilo la Magonjwa ya akili.
 

No comments: