Sehemu ya Majeengo ya Hospitali ya Rufaa mkoani Singida inayokabiliwa na uhaba wa Watumishi wa Afya.
Na Nathaniel Limu, Singida
HOSPITALI
ya Rufaa mkoani Singida,inakabiliwa na uhaba wa watumishi zaidi ya mia
mbili wa kada mbalimbali,kitendo kinachochangia huduma kutokukidhi
mahitaji.
Hospitali
hiyo ambayo ipo nje ya mji wa Singida katika barabara ya Sepuka,kwa
sasa imeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.Huduma zingine ikiwemo ya
akina mama kujifungua,bado hazijaanza.
Hayo
yamesemwa na Afisa Muuguzi wa hospitali hiyo, Pendaeli Masai wakati
akitoa taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone
aliyetembelea hospitali hiyo kujua maendeleo yake.
Amesema
kuwa licha ya hospitali hiyo kuwa na vifaa vya kisasa,huduma
mbalimbali hazijaanza kutolewa kutokana na uhaba mkubwa wa
watumishi.
“Tumeanza
kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje Desemba mwaka jana na kwa kuanzia
tumeanza na watumishi 40 wa kanda mbalimbali.Hawa watumishi
hawatoshi,hali inayopelekea tushindwe kutoa huduma zingine ikiwemo ya
akina mama kujifungulia”,amesema Pendaeli.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Singida.Dk.Parseko Kone,baada ya kukagua
hospitali hiyo,amesema majengo mawili ndiyo yaliyokamilika na mengine
saba yanaendelea kujengwa.
Dk.Kone
amesema yatakapokamilika majengo hayo, inatarajiwa hospitali hiyo
itakuwa na uwezo wa kuhudumia mikoa ya Singida, Tabora, Simiyu, Dodoma,
Shinyanga na Manyara.
Naye
kaimu mganga mkuu mkoa wa Singida, Dk.Musa Kimala amesema kuwa zaidi ya
shilingi milioni 400 zimetumika kununulia vifaa mbalimbali ikiwemo
vitandavya upasuaji,mashine za hewa.
No comments:
Post a Comment