Kijana huyo ambaye anafahamika kutokana na kazi yake ya kukaanga Chips eneo la Ipuli imedaiwa kuwa alimchukua mwanafunzi huyo kwa kumrubuni akampatie nauli ya kupandia baiskeli ili awahi Shuleni majira ya saa mbili asubuhi,na alivyomfikisha nyumbani kwake alimfungia mlango na hatimaye kumaliza haja zake kwa maana ya kumbaka mara kadhaa.
Maelezo yaliyotolewa na mwanafunzi huyo mara baada ya kutafutwa na Mama yake mzazi kwa zaidi ya siku tatu mfululizo ambaye anafahamika kama mama Sabato na hatimaye kupatikana katika mazingira ya kutatanisha,Mwanafunzi huyo aliweka wazi kuwa amekuwa akifungiwa ndani ya Chumba cha Kijana Zakaria ambaye ni mkaanga Chips huku akifanyiwa vitendo hivyo vya kinyama kila siku.
No comments:
Post a Comment