Mama
mzazi wa IGP Ernest Mangu,mkazi wa kijiji cha Kihanuda tarafa ya
Ilongero wilaya ya Singida, Bi. Mwanaidi Msengi akipasua kuni kwa ajili
ya kupikia chakula.
Mama
mzazi wa IGP, Ernest Mangumkazi wa kijiji cha Kihanuda tarafa ya
Ilongero wilaya ya Singida,akiwa amejitwisha chungu akiwa nyumbani
kwake.Mama huyo,amedai kuwa alifanya biashara ya kuuza vyumba na kupata
fedha za kugharamia masomo ya Mangu.
Makazi
ya wazazi wa IGP Ernest Mangu yaliyoko katika kijiji cha Kihanuda
tarafa ya Ilongero wilaya ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya
Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.
.wasema kijiji cha kihunadi alikozaliwa Mangu sasa kujulikana ndani na nje ya nchi
.wasema wamebahatika katika historia yao kutoa kiongozi wa juu katika taasisi nyeti nchini.
.Mama yake Mangu asema alimsomesha IGP kwa kuuza pombe
Na Nathaniel Limu, Singida
UTEUZI
wa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Kamishna Ernest Mangu
umepokelewa kwa nderemo, vifijo na bashasha na wakazi wa kijiji cha
Kihunadi tarafa ya Ilongero wilaya na mkoa wa Singida alikozaliwa IGP
huyo kwa madai kwamba sasa kijiji chao kitajulikana haraka ndani na nje
ya Tanzania.
Wamedai
pamoja na faida ya kujulikana huko,changamoto mbali zinazokikabili
kijiji hicho zitapatiwa ufumbuzi wa kudumu mapema iwezekanavyo.
Wamedai
zaidi kwamba wamekuwa wakiamini kwa Kamishna Mangu atafika mbali katika
kushika nafasi za juu za uongozi kutokana na uadilifu, uchapaji kazi,
ukaribu wake kwa wananchi, uaminifu na uwazi wake.
Kwa
upande wa mama yake mzazi Mwanaidi Msengi, pamoja na furaha kubwa
aliyonayo, amemwasa mtoto wake huyo kuchapa kazi kwa bidii kama njia
mojawapo ya kumshukuru Rais Kikwete kwa kumteua kuwa mzawa wa kwanza wa
mkoa wa Singida, kushika wadhifa huo nyeti.
“Hii
ni heshima kubwa sana kwangu binafsi, ndugu zake, wakazi wa kijiji cha
Kihunadi na mkoa wa Singida, kwa hiyo lengo langu ni kumwombea mtoto
wangu Mangu asimwangushe Rais, atimize wajibu wake ipasavyo ili Rais
Kikwete siku moja aseme hajakosea kumpa Mangu, ukuu wa polisi
nchini”,amesema kwa kujiamini.
Mwanaidi
amesema Mangu alianza elimu ya msingi katika shule ya Kinyagigi,
alikuwa na bidii mno katika kujisomea. Kwenye mitihani mara nyingi
alishika nafasi ya kwanza au ya pili, akifanya vibaya alishika nafasi
ya tatu.
“Mwaka
1977 alifaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga na
elimu ya sekondari katika shule ya Tumaini iliyopo Kinampanda wilayani
Iramba aliyomaliza kidato cha nne”,amesema.
Akifafanua,
Mwanaidi amesema alipofaulu kujiunga na elimu ya sekondari, alilazimika
kuomba ng’ombe kwa mke mweza, ili akamuuze apate fedha za kugharamia
masomo ya mtoto wake.
“Nadhani
mke mwenzangu huyo, alimtoa ng’ombe wake kwa shingo upande kwa sababu
Mangu alipomuuza kwenye mnada pale Singida mjini, aliibiwa fedha zote na
alirudi nyumbani akilia sana”,amesema.
Amesema
baada ya hapo, alimwambia mtoto wake Mangu, kwamba hawataomba tena
ng’ombe na badala yake atatengeneza vyungu kwa kutumia udongo wa
mfinyanzi ili kupata fedha za kugharamia masomo yake.
“Nashukuru
Mangu alinielewa vizuri kwa sababu alishiriki kubeba kichwani vyungu
hivyo wakati wa kuviuza hadi kichwa chake kilikaribia kuwa kipara.
Nilibuni chanzo kingine cha mapato ambacho kilikuwa ni kukoroga na kuuza
pombe”,amesema.
Kwa mujibu wa Mwanaidi, Kamishna Mangu ni mtoto wa pili kati ya watoto saba, aliowazaa.
Aidha,Mwanaidi
ni kati ya wake sita waliowahi kuolewa na baba yake Kamishna Mangu,
Jumbe Omari Mangu, aliyefariki aprili 27 mwaka 1988. Jina la Jumbe
linatokana na kupewa kazi ya ujumbe wa wakoloni wakati wa ujana wake.
Inadaiwa
kwamba baba yake Kamishina Mangu, alioa wanawake hao sita, kwa nyakati
tofauti kwa lengo la kusaka mtoto/watoto wa kiume. Wengi wa wake hao,
walikuwa wanazaa watoto wa kike.
No comments:
Post a Comment