Pages

KAPIPI TV

Friday, January 31, 2014

MBOWE AKAMATWA NA POLISI IRINGA

mbowe 07005
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amekamatwa na kushirikiwa kwa muda Jeshi la Polisi Mkoani hapa akituhumiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wake uliofanyika juzi katika Jimbo la Kalenga Wilaya ya Iringa.

Mbowe alikamatwa majira ya saa tatu asubuhi na kufikishw akatika kituo cha Polisi Wilaya ya Iringa ambapo alihojiwa kwa muda wa saa moja na Dk 45.


Akizungumza mara baada ya kuachiwa Mbowe alisema tuhuma za kuwa yeye amezidisha muda katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mgama jimboni Kalenga si za kweli na kuongez akuwa alikwedna kutuliza hasira za wananchi waliokuw awamesubiri katika eneo hilo kwa muda bila mafanikio.


"Ni kweli tulikuwa na ratiba ya kufanya mkutano katika kijiji kile, lakini mikutano ilikuwa mingi tukachelewa kwa kuhofia hatari ya kusafiri na Helkopta usiku"alisema Mbowe na kuongeza:


Alisema hata baada ya kufika katika eneo lile alimuomba polisi aliyekuwa katika eneo lile kuwa ampatie muda mfupi aweze kuwatuliza wananchi wale waliokuw awamepandw ana hasra baad aya kumsubiri kw amuda mrefu b ila ya mafanikio.


Akizungumzia kukamatwa kwake Mbowe ambaye alikuwa ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee, Mbunge wa jImbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa alisema alikamtwa kikiwa ni mda mfupi baada ya kutaka kuondoka kwenda uwanja wa Ndege wa Nduli kuanza safari ya kwenda mkoani Pwani.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa alisema kitendo kichofanywa na polisi cha kuwakamata viongozi w akitaifa wanapokuw akatika utekelezaji w amajukumu ya kitaifa kinakera na kuwapotezea muda.


"Mimi nilikuwa nyumbani ghafla nikafuatwa na polisi majira ya saa tatu asubuhi nikitakiwa kufika kituoni kw aajili ya kuhojiwa,nasema tu kuwa kitendo hiki kinakera sana,kwani tunamambo mengi yakufanya leo ilikuwa niwe kwenye kikao cha CC cha Mkoa lakini ninapoteza muda hapa,polisi wanaacha kufanya mambo ya msingi wanatumia muda mwingi kutuhoji sisi"alisema Msigwa.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee alisema kitendo cha viongozi hao kushikiriw ana polisi kinaonyesha namna ambapo chama hicho kimekuwa na kutiksa nchi.

Aliwashukuru watanzania kwa kuendelea kuwaunga mkoano huku akisisitiza kuwa wao kushikiriwa na polisi ni kitu cha kawaida.


Mamia wafurika Mwembetogwa kumlaki mbowe
Muda mfupi baada ya mbowe kuachiwa majira ya Saa Nne na Dakika 45, alielekea katika viwanja vya Mwembetogwa ambako uongozi wa chama hicho uliagiza helkopta kuja kumpakia kutoka katika viwanja hivyo na kuelekezwa Pwani.


Mara baada ya kuwasili kwa Helkopita hiyo mamia ya wakazi wa Iringa waliachilia shughuli zao na kufurika katika uwanja huo wakimshangilia Mbowe pamoja na viongozi wengine kwa kufika katika eneo hilo.


Huku wakipiga kelele walisema "Kamanda Mbowe karibu,tunakushuru sana,tunakutakia kazi njema walisikika wakitoa sauti kutoka katika eneo hilo la uwanja na kufanya eneo kuwa kama unafanyika mkutano wa hadhara.


Mbowe ambaye akiwa katika viwanja hivyo alizungumza na waandishi wa habari pia alitumia muda huo kuwaga wakazi wa Iringa na kuwahsukuru kwa kitendo chao cha kukipokea chama hicho Kikuu cha Upinzani.


Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Ramadhan Mungi alithibitisha kutoka akwa tukio hilo na kuongeza kuwa wao kama wasimamizi w amamlaka wataendelea kuwachukulia hatua viongozi wa kisiasa watakaobainika wakivunja sheria za nchi. 

Chanzo: Hakimu Mwafongo

No comments: