Jamii ya watu wa tamaduni za asili na mizimu ya Waswezi mkoani Tabora wameelezea kusikitishwa kwao na hatua ya Chama cha Mapinduzi kutokuwa karibu na watu hao kama ilivyokuwa wakithaminiwa na muasisi wa Chama hicho Mwl.Julius Nyerere enzi za uhai wake.Mmoja wa viongozi wa Kundi la Waswezi amedai kuwa wanashangazwa na viongozi wa CCM kutowahusisha kwenye matukio mbalimbali kama ilivyokuwa hapo awali jambo ambalo alidai kuwa Chama hicho kwasasa kinaonekana kuwatenga bila sababu za msingi.Kiongozi huyo alisema hivi sasa CCM imekuwa ikiwajali Waswezi nyakati za kampeni za uchaguzi tu hatua ambayo alidai hiyo ni moja ya kupoteza historia ya Tabora ambayo Waswezi ni moja kati ya alama zinazoutambulisha mkoa huo.Akirejea kumbukumbu za Mwl.Nyerere alisema,Mwalimu alikuwa hawezi kuja Tabora kabla ya Waswezi kufahamishwa na hivyo kuanza kufanya maandalizi ya mapokezi kwa zaidi ya mwezi mmoja huku Mtemi wa Waswezi marehemu Binti Mpera akiwa na uhusiano wa karibu zaidi na Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere.Jamii ya Waswezi ambayo kwasasa imeonesha kukatishwa tamaa na Chama hicho imekuwa inashindwa kuwaelewa viongozi wa CCM ambao wameshindwa kuzienzi taratibu za kuwaenzi Waswezi kama alivyofanya muasisi wa Chama hicho. |
|
No comments:
Post a Comment