Pages

KAPIPI TV

Friday, November 22, 2013

"UVIMBE WAMTESA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO,AOMBA MSAADA WA MATIBABU"TABORA BOYS

Sehemu ya Uvimbe unaomtesa Mwanafunzi wa kidato cha tano Shule ya Sekondari ya Tabora Wavulana ambaye anafahamika kwa jina la Amos Marko Faida(19)uvimbe huo ambao unatajwa kitaalamu kuwa  kuwa ni TUMOR ON PALATE unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo Saratani  ya kiinywa ambayo itaambatana na kushindwa kusikia na kuona pamoja na kuziba njia ya chakula.
Mwanafunzi Amos Marko Faida ambaye ameanza kupoteza ndoto zake za kuendelea na masomo baada ya madaktari kumpa barua ya kwenda kutibiwa hospitali ya Muhimbili jijini Dar-es-salaam baada ya kushindikana katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora ambapo gaharama za matibabu hayo jumla ya shilingi milioni tano zinahitajika,huku akiwa haoni ni wapi atapata fedha hiyo ikilinganishwa na hali halisi ya maisha yake na namna anavyosoma kwa taabu kubwa. 
Amosi akiwa na mama yake mzazi Bi.Elizabeth Charles wakati walipotembelea ofisi ya Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Tabora kutaka umma ufahamu juu ya tatizo linalomkabili Mwanafunzi Amosi.Sambamba na hilo kwa mtu yeyote atakayeguswa na kutaka kumsaidi Mwanafunzi huyo awasiliane kwa simu namba 0752 983871 au atakayetaka kumchangia mwanafunzi huyo anaweza kuwasilisha michango yake kwa njia ya M-PESA au AC. NMB :5152402049 au afike na kumuona Mwanafunzi huyo shuleni kwake Tabora Boys kidato cha tano PCM.






No comments: