Pages

KAPIPI TV

Tuesday, October 1, 2013

"POLISI ATAKAYEWASUMBUA BODABODA SASA KUKIONA"-RC FATMA MWASSA

Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa  akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya Chama Cha Waendesha Bodaboda mkoa wa Tabora TTMA zilizopo eneo la Bachu kata ya Gongoni manispaa ya Tabora.Katika ufunguzi wa Ofisi hiyo pamoja na mkuu huyo kuwataka waendesha Bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani lakini akatumia fursa hiyo kukomesha vitendo vya baadhi ya askari Polisi wasio waaminifu kutowafanya waendesha Bodaboda kuwa sehemu ya kipato chao kwa kuwalazimisha kutoa rushwa baada ya kuwabambikiza makosa wasiokuwa nayo.Aidha  Bi.Fatma Mwassa alisema serikali haitakubali kuvumilia vitendo vya kuwanyanyasa  Bodaboda ambao wamekuwa wakijitafutia riziki zao kwa kufanya shughuli hiyo ya halali.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa ofisi hiyo ya  Chama cha Waendesha Bodaboda Tabora,kushoto ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Waziri Kipusi.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akipata maelezo ya uendeshaji wa ofisi ya Chama cha Waendesha Bodaboda Tabora,hapa alikuwa akiangalia orodha ya wanachama ambao inaonesha mahali wanapoishi,takwimu za ajali pamoja na mahusiano yao na Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa,mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Suleiman Kumchaya,viongozi wa chama cha Waendesha Bodaboda Tabora  pamoja na wanachama hai wa Chama  hicho muda mfupi mara baada ya ufunguzi rasmi wa ofisi hiyo.  


No comments: