Pages

KAPIPI TV

Sunday, September 1, 2013

MTOTO ANAOMBA MSAADA WA PESA KWA AJILI YA KUKATWA MIKONO YAKE,IMEANZA KUHARIBIKA-0766 346407

Mtoto huyu anayefahamika kwa jina la Hamisi (13)ambaye kwasasa amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete wadi na moja ,anaomba wasamalia wema kumsadia apate fedha za matibabu ya mikono yake yote miwili ambayo iliathiriwa vibaya na umeme mkali wa Transifoma mahali ambako mtoto huyu alikuwa akicheza na kujikuta akipigwa shoti na umeme huo mkali.Kwa mujibu wa madaktari wa hospitali hiyo wamedai kuwa huduma pekee kwa majeraha ya mtoto huyu ni kukatwa mikono yake yote miwili ambayo tayari imeanza kutoa wadudu kwa maana ya kuoza.Aidha kwa wanaotaka kumsaidia mtoto huyu wanaweza kufika hospitalini hapo au kuwasiliana kwa simu namba 0766346407 namba ambayo pia waweza kutuma msaada wako kwa njia ya M-PESA,kwakuwa mikono ya mtoto huyu pia imekuwa ni hatari kwa afya yake na wagonjwa wengine katika wadi hiyo.


No comments: