Risasi 60 zilizokamatwa kwa Robert Maziku mkazi wa Mwanzaroad Tabora mjini. |
Na Juma Kapipi Tabora.
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Robert Maziku(40) mkazi wa Mwanzaroad manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kumkuta na risasi 60 za bunduki aina ya SMG isivyo halali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Peter Ouma aliueleza mtandao huu kuwa kukamatwa kwa risasi hizo ni matokeo ya msako wa mara kwa mara unaofanywa na Jeshi hilo kupambana na vitendo vya kiharifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tabora.
Alisema mnamo tarehe 5/7/2013 majira ya saa nane usiku huko barabara ya Sikonge manispaa ya Tabora,Robert Maziku alikamatwa na risasi hizo alizokuwa amezihfadhi kwenye kibegi kidogo cha mgongoni akiwa anataraji kuzipeleka kusikojulikana kwa ajili ya kufanyia uharifu.
Kamanda Ouma ambaye alitamba tayari mtuhumiwa huyo Maziku amekwisha fahamisha Polisi mahala ambako Bunduki wanayoitumia wameihifadhi yeye na wenzake ambao hata hivyo hakutaka kutaja majina yao.
Aidha sambamba na kukamatwa kwa risasi hizo Ouma alisema Jeshi hilo wamekamata silaha aina ya Shortgun yenye nambari 00NN094188 ikiwa imetelekezwa shambani katika kijiji cha Busodi wilayani Kaliua baada ya msako mkali uliojumuisha askari Polisi na wananchi.
Katika wilaya ya Urambo zoezi la msako huo mkali ulifanikiwa kumtia nguvuni Katondo Paul(49)mkazi wa kijiji cha Mirambo tarafa ya Ussoke akiwa anamiliki silaha aina ya Gobore 1,vipande vya gololi 28,baruti kilo 5,watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment