Joyce Kiria mke wa Bw.Kilewo akiwa na baadhi ya makamanda wa Chadema ndani ya ukumbi wa Mahakama kuu kanda ya Tabora wakisubiri kuanza kwa mahakama hiyo.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo makamanda walipakizwa ndani ya gari tayari kwa kurejeshwa mahabusu Gereza la Uyui mkoa wa Tabora. |
Mahakama kuu
ya Tanzania kanda ya Tabora imeahirisha usikilizwaji wa shauri la jinai
linalowakabili wanachama watao wa Chama cha Demokrasia na Maendelo – CHADEMA –
hadi tarehe 30 mwezi huu baada ya kutokea ubishani hoja za kisheria kati ya
wakili wa serikali na wa utetezi.
Uamzi huo
umefikiwa na jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Simon Lukelewa mara baada ya
kukubaliana na maombi ya wakili wa serikali Juma Masanja kwamba walichelewa
kupata nakala ya maombi yaliyowasilishwa mahakama kuu na wakili wa washitakiwa.
Katika
maombi yake wakili wa serikali aliiambia mahakama hiyo kuwa wao walipokea
nyaraka hizo tarehe 19/07/2013 hivyo
haikuwa rahisi kuweza kuzijibu na pia
aliomba wapewe nakala za mashauri mawili yaliyofunguliwa katika mahakama
za wilaya ya Igunga na ile ya hakimu mkazi wa mkoa dhidi ya wanachama hao wa Chadema.
Wakili
Masanja aliiomba mahakama hiyo isiendelee kusikiliza rufaa hiyo ya mombi ya marejeo namba 53/2013 na iwape
mda ili waweze kujibu hoja zilizo wasilishwa na upande wa utetezi .
Katika
maombi yao yaliyowasilishwa na wakili Peter Kibatala waliiomba mahakama kuu
ipitie majalada ya kesi hizo mbili na hiyatolee maamuzi kwani inaonekana
wameshindwa kutimiza wajibu wao.
Wakili
Kibatala ameainisha katika maombi hayo kwamba kutokana na maamuzi hayo ya
mahakama za chini yameathiri pia haki za waomba rufaa ikiwemo kupata dhamana.
Akitoa
maamuzi ya hoja za mawakili hao aliutaka upande wa serikali uwe umejibu hoja
hizo kabla ya tarehe 29/07/2013 ili ifikapo julai 30 aweze kutoa maamuzi na kupanga tarehe ya kuanza usikilizwaji wa
shauri la maombi ya marejeo lililowasilishwa na wakili Kibatala.
Watuhumiwa hao watano akiwemo kaimu katibu wa chama hicho mkoa wa Dare salaam Henry
John Kileo wanakabiliwa na mashitaka
mawili kuwa tarehe 09-09-2011
walimjeruhi bwana Mussa Tesha kwa
kutumia tindikali na pia kutenda vitendo vya kigaidi chini ya kifungu cha nne
cha sheria.
Wanachama
wengine wa CHADEMA wanaokabiliwa na mashitaka hayo mawili ni pamoja na Evodius
Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta n Rajab Kihawa.
Akizungumza
nje ya Mahakama,Wakili wa washtakiwa hao,Peter Kibatala,alisema amefurahishwa
na maamuzi yaliyotolewa na jaji kwa kuonyesha kutenda haki kama ambavyo
walivyotarajia kupata toka Mahakam hiyo ya juu.
Kwa upande
wake Mke wa mshtakiwa Henry Kilewo, Joyce Kiria,ambaye alifika mahakamani hapo
kufuatilia kesi ya mumewe aliwasisitiza wanawake wenzake kuwa wavumilivu wakati
ambapo famiria zao zinapokuwa katika misuko suko ya kimaisha.
Alisema yupo
naye katika kipindi hiki na bado anampenda na kuwatia moyo wanawake kuwa begakwa
bega na waume zao pale wanapokumbwa na
matatizo.
Shauri hilo
lilivutia umati wa wapenzi wa CHADEMA waliojitokeza kwa wingi huku ulinzi ukiwa
mkali ambapo Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia walitanda wakiwa na silaha.
No comments:
Post a Comment