Na Mwandishi wetu,Tabora
VIONGOZI wa baadhi ya vyama nchini wameonywa kuacha tabia ya kuhubiri
maneno ya kuwagawa watanzania kwa misigi ya rangi, ukabila na udini.
Hayo yalisemwa na mlezi wa chipukizi na Green Guard wilaya ya Tabora
mjini Emmenuel Mwakasaka, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata
ya Kakola ikiwa ni ziara ya jumuiya ya UVCCM wilaya ya Tabora mjini,
katika kuimarisha umoja huo.
Mwakasaka alisema kwa muda mrefu watanzania wameishi bila kujali
rangi, udini na ukabila huku wakiishi kwa kuvumiliana kwenye tofauti
hizo.
Aidha alisema hivi sasa wapo baadhi ya viongozi wameanza kumomonyoa
maadili ya utaifa tulionao kwa kipindi kirefu ambao tumeachiwa kama
urithi na waasisi wa taifa hili.
Alisema viongozi hao wa kisiasa wamekuwa na ajenda tofauti katika
kugawa watanzania kwa maslahi yao binafsi napenda ifikie mahali watu
hao wakemewe kwa nguvu zote na wananchi kuwapuuza.
“Niwasihi tu watanzania wenzangu na viongozi kuuenzi utamaduni wetu
hususani vijana wadogo kama chipukizi ambao yeye ni mlezi wao.”alisema
Mwakasaka.
Aidha aliwataka vijana kuwa makini na baadhi ya wanasiasa wenye tamaa
ya madaraka,na kwataka kuwa na uzalendo,kuipenda na kuwa tayari
kuitumikia nchi yao wakati wote.
Aidha aliongeza kuwa ifikie mahali baadhi ya sisi viongozi kuachana na
propaganda chafu za kisiasa ambazo athari zake ni kubwa na kuwe na
utayari wa kutumikia watanzania kwenye nyanja za kiutamaduni,kisiasa
na kijamii.
Aidha alionya viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa kuacha kuudanganya
umma hasa vijana kuwa watawaletea maendeleo huku wakijua kuwa
maendeleo yanaletwa katika pande mbili ambazo ni serikali na
watekelezaji ni wananchi wenyewe.

No comments:
Post a Comment