Jeshi la Polisi Zanzibar Jumamosi Juni 15, 2013 litafanya matembezi (Route March) ya pamoja kati yake na Askari wa Vikosi vya SMZ.
Kamishna
wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, ameyataja makundi mengine
yatakayoshiriki kwenye matembezi hayo kuwa ni pamoja na , Vikundi vya
Mazoezi ya Viungo pamoja na Vikundi vya Ulinzi Shirikishi.
Amesema
matembezi hayo ambayo yataanza saa 12.00 alfajiri siku hiyo, yataanzia
kwenye Viwanja ya Polisi Ziwani na kuishia nje ya Uwanja wa Michezo wa
Amani saa 3.00 asubuhi.
Kamishna
Mussa amesema matembezi hayo yenye sura ya amani yatapokelewa na Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Maghari Unguja Bw. Abdallah Mwinyi Khamisi na washiriki
wake watatoka katika mikoa mitatu ya Unguja.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Kamishna Mussa amewaomba wananchi
wa mji wa Zanzibar na Viunga vyake wameombwa kufika nje ya Uwanja wa
Amani kuanzia saa 2.00 asubuhi ili kupata ujumbe utakaotolewa siku hiyo.
Viongozi mbalimbali kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar watahudhuria katika mapokezi hayo.
Aidha
Waandishi kutoka vyombo mbalimbali wa Habari, wameombwa kuhudhuria ili
kusaidia kutoa elimu kwa umma juu ya yale yote yatakayoelekezwa kwa
manufaa ya Taifa letu.
IMETOLEWA NA INSP. MOHAMMED MHINA, AFISA HABARI MKUU WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR.
0715 886488, 0784 886488, 0767 886488
No comments:
Post a Comment