Naibu Katibu mkuu bara wa Chadema na mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika viwanja vya Stand ya zamani manispaa ya Tabora. |
Na Hastin Liumba,Tabora
KITENDO
cha naibu katibu mkuu bara wa chama cha demokrasia na maendeleo,
(CHADEMA),Zitto Kabwe kutamka hadharani kwenye mkutano wa hadhara kuwa
wabunge wa CCM mkoani Tabora ni wasaliti,wanafiki na watoro kwenye
majimbo yao, kimepokelewa kwa hisia tofauti na wapiga kura wakiunga mkono
kauli hiyo.
Kabwe
alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya
mabasi zamani, ikiwa ni sehemu ya ziara yake kuimarisha CHADEMA kanda ya
magaharibi yenye mikoa ya Tabora,Katavi na Kigoma.
Aidha
mbunge huyo alisema wabunge hao wamekuwa wakiwasaliti wapiga kura hasa
kwenye miradi ya maendeleo kwani hivi karibuni walijpanga kukwamisha
bajeti ya wizara ya ujenzi inayoongozwa na Dk. John Magufuli,lakini waliitwa
na waziri mkuu Mizengo Pinda na kukalipiwa kutofanya hivyo.
Wabunge
wa majimbo ya mkoa wa Tabora,ni Ismail Rage (Tabora mjini),Shaffin
Sumar (Tabora Kaskazini), Samweli Sitta (Urambo),Profesa Juma Kapuya
(Kaliua),Dk Athuman Mfutakamba (Igalula),Suleiman Zedi (Bukene),Dk Hamis
Kigwangalah (Nzega),Said Nkumba (Sikonge),na Dk Dalali Kafumu (Igunga),
ambaye amerejeshewa ubunge wake na mahakama kuu kanda ya Tabora.
Aidha wabunge wa viti maalumu CCM Tabora kwa tiketi ya CCM ni Munde Tambwe na Magreth Sitta.
Alisema alifikia mahali akawa anawashangaa wabunge hao wa CCM kila aliyesimama aliunga mkono hoja kwa asilimia 100.
Kutokana
na kauli ya Zitto kudai ni wasaliti na watoro majimboni mwao hata wale
wa viti maalumu,baadhi ya wananchi baada ya mkutano huo wa hadhara
walionekana kwenye vikundi sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za starehe
kama baa,vijiweni wakijadili na kukubaliana na kauli ya Zitto.
“Jamani
kauli ya Zitto ni ya kweli hebu angalieni wabunge karibu wote utawaona
wanakuja mara chache sana majimboni na wanaweza kuja na wasifanye
mikutano yoyote na wananchi.”alisema kijana mmoja ambaye anayefahamika kwa jina la
Haruna.
Walisema
wanaungana na kauli hiyo ya utoro kwani hata kwenye vikao vya DCC na
RCC ni nadra sana wabunge hao kuhudhuria mara kadhaa ukisoma kwenye
muhtasari utaona labda ni mbunge mmoja tu alikuwepo wengine wote ni
udhuru kwa kwenda mbele.
Kiongozi
mmoja wa chama siasa cha NRA Nkumila, alisema yeye vikao vya kamati za
ushauri za wilaya na mkoa yaani DCC na RCC mjumbe halali lakini wabunge
wengi hawahudhurii kabisa sasa mkoa utapataje maendeleo ikiwa yale
yanayojadiliwa hawayasikii ili wakasaidie kwenye kikao kama cha bunge.
Aidha
wakazi hao walionekana kukunwa na kauli ya Zitto wakisema alichosema
kina ukweli na kwamba baadhi ya miradi ikikamilika kwa haraka
itakuwa nguvu ya CHADEMA kwani wabunge wa CCM wanazibwa midomo wasipige
kelele kwa kigezo wa kuibomoa serikali yao.
Hali
hiyo waliendelea kujadiliana hata katika maeneo kadhaa mjini hapa wakidai
wamechoshwa na wabunge wa kuja hata wale waliojifanya wamezaliwa Tabora
siku hizi wamehamia jijini Dar-es-Slaam kwenye shughuli zao binafsi.
Walisema
wanatafakari kwa umakini mkubwa maneno ya Zitto kuwa Tabora CCM
imepafanya ni sehemu ya kuchota kura na kamwe wataendelea kubaki kama
walivyo kwenye kisiwa na hawajui lini wataokolewa labda pale
watakapofanya maamuzi magumu ya kuitosa CCM 2015.
Wakati
wananchi wakijadiliana hayo na wengine kuongea na waandishi wa habari
tayari mwenyekiti wa CCM taifa,Dk Jakaya Mrisho kikwete kwenye kikao cha
wabunge wa CCM amekemea tabia ya wabunge watoro wasiotembelea majimbo
yao.
Katika
kikao hicho kilichofanyika mjini Dodoma, rais alisema kuwa baadhi ya
wabunge wameyatelekeza kwa kutorudi kusikiliza kero za wananchi na
kutimiza ahadi zao.
Aliwaonya kuwa kwa tabia hiyo wala wasije kuwaonea donge wale wanachama wengine watakaochaguliwa kuwa wabunge badala yao.
No comments:
Post a Comment