Habari zilizotufikia muda huu
zinaripoti kwamba hali sio nzuri huko Mtwara, kwa ufupi hali ni tete na
hakuna amani, mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za
kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote
zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla
kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi
wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali
nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
Kufuatia
Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la
gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma
hotuba yake.
Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto.
Lodge/Hotel
(Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la
Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea
imechomwa moto.
Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani. (habari haijathibitishwa rasmi)
Ni
magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu
kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi.
Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa muda huu Bungeni.
No comments:
Post a Comment