Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 29, 2013

MJENGWA AIBIWA CAMERA NA SIMU,CHUMBA KILIPULIZIWA SUMU YA USINGIZI,WEZI WALISHIRIKIANA NA WALINZI

6 444e6
Ndugu zangu,
Usiku wa kuamkia leo nimepatwa na bahati mbaya ya kuibiwa  kamera  ( Pichani) na simu yangu aina ya Samsung Galaxy S4. Vyote hivyo ni kama jembe na nyundo zangu.
Ilikuwaje? Nilifika Msamvu nikitokea Iringa jana jioni. Baada ya mlo wa usiku nikaingia chumbani kwangu mahali nilipofikia. Nikafanya kazi mpaka saa tano na nusu. Nilitaka nilale mapema kwa kujiandaa kwa safari ya alfajiri ya leo kuwahi Dar kwenye mikutano ya kazi.

Kabla alarm yangu haijalia ya saa kumi na nusu alfajiri nikaamshwa na sauti za watu wanaume wawili wakiongea nje ya dirisha langu. Nilipochungulia nje dirishani nikaelewa  kuwa kuna wizi umetokea.  Watu wale wakaondoka ghafla. Walikuwa ni walinzi. Kisha wakarudi baada ya dakika kumi na kuniambia kuwa " Bwana Mjengwa umeibiwa!" Jambo ambalo nilishalibaini mwenyewe.

Kwamba sikuibiwa kamera na simu tu, na wallet yangu pia iliyokuwa na kiasi cha fedha ndani yake. Bahati nzuri wezi wale walichukua fedha na kuniachia wallet ikiwa na vyote muhimu ikwamo kadi za benki na hata kitambulisho changu cha Mpiga Kura.

Inavyoonekana, wezi wale wali spray chumba changu na kunifanya nilale muda wote wakifanya uhalifu wao. Maana, kawaida yangu hushtuka haraka kwa milio ya ajabu usiku na hata mwanga wa tochi. Na ajabu ya wizi waliofanya chumbani kwangu, walifanya hivyo hivyo kwenye chumba cha ndugu yangu Daniel Londo, mkewe na mtoto wa mwaka mmoja na nusu.  Walitumia mti na kutengeneza kitu kama ndoano. Inaonekana waliweka gundi pia kwenye ndoano ile, kisha wakapenyeza dirishani.

Tunashuku kuwa wezi walishirikiana na walinzi wawili wa usiku mahali hapo nilipofikia. Leo asubuhi, mimi na Daniel Londo tumeripoti tukio hilo Kituo Kikuu Cha Polisi, Morogoro.
Ndugu zangu,

Hapo Morogoro katika pitapita zenu huenda mnaweza kumwona anayeuza mtaani kamera aina  ya Canon D35,  yaweza kuwa kamera ya Mwenyekiti wenu, na simu pia, niliyoitaja hapo juu.

Maggid,
Dar es Salaam
0754 678 252

No comments: