Na Mwandishi wetu.
Wakati
bado wakazi wa dubai hawajasahau kufunguliwa kwa jengo refu kuliko yote
duniani..kiongozi wao ametoa kali nyingine,Al maktoum aligawa new mode
lamborghini aventador katika vituo vya polisi ili zitumiwe katika
patrol..kabda ya hapo polisi walikuwa wakitumia prado suv na bmw 5
series,
Nchi ya Qatar ndio ilikuwa ya kwanza kwa polisi wake kutumia
lamborghini kama magari ya patrol,katika hotuba yake al maktoum alisema
ameamua kutoa lamborghini na ferrari kutokana na spidi nzuri ya magari
hayo..lamborghini ina spidi ya 217mph.
Polisi wa hapa dubai wanaishi maisha mazuri kuliko fani nyingine
nyingi na ndoto ya vijana wengi walio vyuoni na shuleni ukiwauliza
wanasema wanataka kuwa polisi,katika pitapita zangu niliwahi kuulizia
mshahara wa polisi nikaambiwa kwa kuanzia ni almost 35,000/ dhs ambazo
ni sawa na tsh 15ml..pia wana huduma zote..ukienda kwenye vituo vyao
utakuta magari na pikipiki nyingi kuliko ata namba ya polisi wenyewe..
Wakati mwingine mimi siwalaumu polisi wetu wa bongo maana maisha yao
tunayajua....usiongelee vifaa vya kazi bali ata uniform tu ni
tatizo,tazama viatu!!nyumba zao!!wakiomba chai huwa sishangai ata
kidogo..maana mtu hajui kesho atakula nini!!!!
No comments:
Post a Comment