Pages

KAPIPI TV

Monday, April 29, 2013

MKUTANO WA CHADEMA WAIBOMOA CCM TABORA

Na Mwandishi wetu maalum,Tabora

CHAMA cha demokrasia na maendeleo kimedhihirisha kuwa bado ni chaguo la Watanzania walio wengi kwa kuendelea kukubalika kila kona ya nchi licha ya upinzani mkali wanaopata kutoka kwa chama tawala, ambapo kimebainisha kuwa propaganda za CCM dhidi yake hazitafanikiwa na badala yake kitaendelea kusimama na kuwatetea wananchi kwa nguu zake zote.
Hayo yalibainishwa na mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe wakati
akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu kwenye viwanja vya shule ya msingi Town School katika manispaa ya Tabora.

Mbowe alisema kuwa CCM baada ya kuona hali ni mbaya kwao wameamua kuanzisha propaganda za kukichafua CHADEMA kwa kudai kuwa ni chama cha wakristo, magaidi na ni chama cha wachaga hivyo hakifai kuongoza nchi.

Mbowe alisema hivi sasa CCM wamegundua kuwa mwaka 2015
hawatatoka na hivyo wamekuwa wakiibuka na program kadhaa dhidi ya CHADEMA ili kukidhoofisha lakini kamwe hawatafanikiwa kwani chama hicho kiko imara zaidi.

Aidha, Mbowe alitolea mfano wa vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF jinsi vilivyopakaziwa udini na ukabila ili kuvidhoofisha na hatimaye visambaratike na sasa wamehamia
CHADEMA, lakini hawataweza, badala yake wanazidi kutuimarisha zaidi, watashangaa matokeo ya mwaka 2015 kwenye uchaguzi.

Aidha aliongeza kuwa propaganda zao zimekufikia mahali wanatumia
vyombo kadhaa vya ulinzi na uslama na zaidi wao kama CHADEMA wameendelea kujipanga vyema na na kwa kuwahakikishia kuwa watafanikiwa vita hii kwa sababu Mungu yupo pamoja nao.

“Ndugu zangu Watanzania tunahitaji kuungana……sisi pekee hatuwezi, naomba wasomi wote, wakulima, waalimu, wafanyabiashara, wakiwemo usalama wa taifa, polisi , JWTZ na wananchi wote, ili tuweze kuikomboa Tanzania , kwani kama ni kupigika kimaisha tumepigika wote.

Akishangiliwa na umati mkubwa wa watu Mbowe alisema kuwa nchi yetu i hoi kiuchumi
kiasi kwamba inashindwa hata na nchi zilizokuwa nyuma yetu kiuchumi ambapo sasa nchi hizo ziko vizuri wakati Tanzania tukiendelea kusuasua na umasikini wetu japo tunazo raslimali tele.

Mbowe alisema yako mambo ambayo Watanzania wakiyasikia wanaweza wakatokwa

na machozi akitolea mfano wa viongozi waastaafu tisa ambao wametengewa sh.bilioni 12, huku kila mmoja wao akilipwa mshahara mnono kwa mwezi ambapo

ukizigawanya kwa mwaka unapata kiasi cha sh milioni 920 kwa kila mmoja
anazopata.
Alisema haya mambo yanafahamika ndani ya wabunge na ndiyo maana
wanasema iko siku mle bungeni zitapigwa kavukavu, huku akiwapongeza

wabunge wa upinzani na wachache wa CCM waliosimama kidete kuondoa hoja
ya maji.

Alisema endapo wananchi wataendelea kuikumbatia CCM hakuna mabadiliko
yoyote yatakayokuja hata tukiweka manabii wa ukweli kama mfumo ndiyo huu huu, haitasaidia na ana imani siku CCM itakapoondoka madarakani
watasambaratika.

Naye mbunge Zitto Kabwe alisema serikali ya CCM imefikia mahali
imekalia taarifa za utendaji wa CAG ambapo amesema fedha za walipa kodi zinatafunwa
na watumishi wa umma na serikali imegoma taarifa hiyo isijadiliwe
Kabwe aliongeza kuwa hivi sasa kutokana na serikali ya CCM kushindwa
kuongoza dola imekuwa kama Tanzania tumerudi nyuma miaka 20 kule tulikotoka kiuwajibikaji , hali ambayo ni hatari sana.


Katika ziara hiyo mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alizindua
uhai wa chama hicho kwa kuweka utaratibu wa kufungua matawi kila mtaa
na Zitto kupewa ulezi wa program hiyo ambapo itatengwa ratiba kila
mwishoni mwa wiki kufanya kazi hiyo hadi kieleleweke.
Katika mkutano huo makada wawili wa CCM walitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA akiwemo katibu wa UVCCM wilayani Uyui na mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoani Tabora, Lumola Steven Kahumbi, na kada mwingine ni  Moses Singu, aliyekuwa diwani wa CCM kata ya Itonjanda katika Manispaa ya Tabora mwaka 2000-2005 na mwenyekiti wa UVCCM Tabora mjini  2003-2008 .

No comments: