Pages

KAPIPI TV

Wednesday, March 13, 2013

UFUGAJI NYUKI UTAWAKOMBOA WANANCHI WA SIKONGE-DC.

“Tunahakika mipango tuliyonayo inaweza kumaliza umasikini kupitia asali”.

Na Hastin Liumba,Sikonge

WILAYA ya Sikonge ni moja kati ya Wilaya sita za Mkoa wa
Tabora,wilaya hii  iko umbali wa kilomita 80 kusini, toka makao makuu
ya Mkoa, eneo la Wilaya  ni kilomita  21,000.

Utawala

Wilaya ina tarafa mbili kata 17 vijiji 64 na vitongoji 241,kwa mujibu
wa  sensa ya mwaka 2002, wilaya ilikuwa na watu 134,000 mpaka kufikia
desemba  2012, inakadiriwa kuwa na wakazi 184,662.

Eneo hili linajumuisha maeneo mbalimbali kama vile maeneo ya makazi,
kilimo, misitu ya hifadhi, misitu isiyohifadhiwa, maeneo ya
wanyamapori  (Game Reserves), vyanzo vya maji (mabwawa, mito pamoja na
marambo), wilaya  ina jumla ya misitu tisa (9), misitu  minne  ni ya
serikali kuu na mitano  ni ya Halmashauri ya wilaya.


Mkuu wa wilaya ya Sikonge, Hanifa Selengu,alifanya mahojiano na
mwandishi  wa makala hii,ofisini kwake na kueleza mkakati wake katika
suala la ufugaji  wa nyuki, hasa kutokana na asali inayozalishwa
wilayani humo kuwa na  ubora  wa hali ya juu.

Maendeleo ya ufugaji nyuki

Selengu anafafanua kuwa misitu kadhaa hutumika kufanya shughuli za
ufugaji  nyuki, zaidi ya asilimia 90,  ya shughuli hizo hufanyika
ndani ya misitu ya  hifadhi  wafugaji huingia katika misitu hiyo kwa
vibali vinavyotolewa na  Idara ya maliasili kuanzia mwezi wa sita hadi
mwezi wa kumi na mbili kila mwaka,vibali hivyo huwa na muda wa miezi
mitatu mitatu ili kuepusha watu  kurundikana ndani ya mapori hayo.

Aidha mkuu huyo wa wilaya anaongeza kuwa hadi sasa wapo wafugaji 785
wa  nyuki,  ambao wameunda vikundi vya ufugaji nyuki,vyama vya ufugaji
nyuki na  vikundi  vya wafugaji nyuki  vipo 11 vyenye wanachama 212
wanawake 49 na wanaume
163, aidha vipo vyama vya wafugaji nyuki 10 vyenye wanachama 573
wanawake  60 na wanaume 512, Hivyo kuleta idadi ya wafuga nyuki 785.



Selengu anataja vyama 10 vya wafugaji nyuki vyenye wanachama 573,
ambavyo ni Kiwani (Ipole),Usenga (Mission),Kitunda (Kitunda),Chabutwa
(Chabutwa),Ugunda (Utimule),Igavanapina (Kiloleli),Safari
(Mkolye),Kiloli(Kiloli),Pata  asali (Igigwa) na Mapambano (Kipili).

Idadi ya Mizinga

Selengu anaongeza kuwa wafugaji hutumia mizinga ya magome, magogo, na
masanduku,ambapo Mizinga ya kisasa mwaka 2005 ilikuwa 398 na  mwaka
2012  imeongezeka na kuwa mizinga 5,316,halikadhalika mizinga ya
kienyeji mwaka  2005 ilikuwa 45,691  na mwaka 2012 mizinga ya
imeongezeka kufikia 84,243.

Aidha aliongeza mizinga ya magome imepungua kutoka mizinga 40,920
mwaka  2005 hadi mizinga 13,306 kwa mwaka 2012, ambapo lengo lililopo
ni kupunguza mizinga ya kienyeji kwa asilimia 80.

Uzalishaji.

Mkuu huyo wa wilaya anasema kuwa Mizinga ya kisasa 5000, huzalisha
asali  lita 10,000 ukilinganisha na mizinga 5000 ya kienyeji ambayo
itazalisha  asali lita 4000 hadi 5000 hili ni ongezeko la zaidi ya
mara mbili.

Uzalishaji wa mazao ya nyuki 2005 – 2012.

Selengu anabainisha kuwa uzalishaji wa mazao ya nyuki umekuwa
ukiongezeka toka mwaka 2005 hadi 2012, ambapo mwaka 2005 jumla ya tani
40 za asali  zilizalishwa zikiwa na thamani ya sh milioni 33,325,000
na mwaka 2012 jumla  ya tani 210 zilizalishwa zikiwa na thamani ya sh
milioni 560,000,000.

Aidha Selengu anaongeza kuwa mwaka 2005 jumla ya tani 1.3 za nta
zilizalishwa zikiwa na thamani ya sh milioni 1,056,000 na mwaka 2012
jumla  ya tani 8 zimezalishwa zenye thamani ya sh milioni 31,548,000 .

Vyama vya ufugaji nyuki.

Selengu anasema toka mwaka 2005-2012 kuna idadi ya mizinga
iliyoongezeka  ambapo  2005 magogo  4,771,magome  40,920  na sanduku
398,2006 magogo  5,364,magome 35,610 na Sanduku ni 569,2007 magogo
5,960,magome 21,071,na  sanduku 814, 2008 magogo 13,083,magome 19,175
na sanduku ni 1,237, 2009 magogo 66,180 magome 14,253, na sanduku
4,306.

Aidha aliongeza mapema mwishoni mwa mwaka 2012,mkuu wa mkoa wa
Tabora,Fatma Mwasa alikabidhi idara ya maliasili wilaya ya
Sikonge,jumla ya mizinga ya kisasa 130,ambapo mizinga 30 ilienda kituo
cha ufugaji nyuki kata ya Ipole,100 ilikwenda kikundi cha vijana kata
ya Lufisi

Aidha anaongeza zaidi kuwa 2010 magogo 68,227, magome 13,705, na
sanduku  4,955 mwaka 2011 magogo 70,337,magome 13,306 na sanduku
5,085, 2012 magogo  5,316,magome 70,937 na sanduku ni 13,306.

Mafanikio ya ufugaji nyuki 2005 -2012.

Selengu anafafanua kuwa katika shughuli ya ufugaji nyuki kumekuwa na
mafanikio katika nyanja mbalimbali kwa kuongezeka kwa pato la wafugaji
wa  nyuki toka sh milioni  33,325,000 mwaka 2005, hadi sh milioni
592,0000,0000 mwaka 2012 ambapo haya ni mapato yatokanayo na asali
pamoja na nta.

Aidha anaongeza kuwa ongezeko la wafugaji nyuki na hadi kufikia mwaka
2012  wapo wafugaji nyuki wapatao 785 ambao wameunda vikundi vya
ufugaji nyuki au  vyama vya ufugaji nyuki.

Alisema vikundi vya wafugaji nyuki  vipo 11 vyenye wanachama 212
wanawake  49 na wanaume 163, aidha vipo vyama vya wafugaji nyuki 10
vyenye wanachama  573 wanawake 60 na wanaume 512, Hivyo kuleta idadi
ya wafuga nyuki 785.

Alivitaja vikundi hivyo na mahali vilipo kuwa ni Lekatugeme
(Lukula-Kitunda),Uhai-Mazingira (Sikonge),Jahazi (Sikonge),Maendeleo
(Kapumpa-Kitunda),Mkombozi(Mkola-Kitunda),Nyahua
(Sikonge),Nsengila(Chabutwa),Tumaini (Urafiki-Usunga),Femash Honey
(Sikonge), Honey (Mtakuja) na Tupendane (Chabutwa) ambapo wanachama
wake  wapo 212 ,wanawake 49 na wanaume 163.

Ujenzi wa vituo vya kukusanyia asali.

Mkuu huyo wa wilaya anabainisha kuwa hadi sasa wilaya imefanikiwa
kujenga  vituo vya kukusanyia asali 3, Kituo cha kukusanya na
kuchakata mazao ya nyuki kilichopo kata ya Ipole, katika ofisi ya
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanayamapori Ipole (JUHIWAI).

Aidha anaongeza kuwa kuna Kituo kingine cha kukusanya mazao ya nyuki
kilichopo kata ya Ngoywa, katika kijiji cha Utimule chini ya usimamizi
wa  JUHIWAI, na Kituo cha kukusanya asali kilichopo kata ya Sikonge
kijiji cha  Mlogolo,na kuna ujenzi wa vituo 2, vinavyotumiwa na VGS
kulinda rasilimali za maliasili vya Ikanjagala na Utimle.



Ongezeko la idadi ya mizinga ya kisasa.

Selengu anabanisha kuwa, ongezeko la idadi ya mizinga ya kisasa toka
mizinga 398 mwaka  2005 na kufikia mizinga 5,316 kwa mwaka 2012 na
mizinga  ya magogo imepungua toka mizinga 40,920 mwaka 2005,hadi
mizinga 13,306, 2012, kwani imeonyesha mizinga hiyo huharibu
mazingira.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya anasema anayo mikakati ya
kuanzisha shamba darasa 1 (Demostration Apiary), katika kata ya
Kiloleli itakayotumika katika utoaji wa elimu ya ufugaji endelevu kwa
kutumia mizinga ya kisasa.

Alisema hadi sasa wafugaji nyuki wamepata  mafunzo ya ufugaji nyuki
kisasa,mafunzo ya kutumia mavazi ya kinga katika chama cha ufugaji
nyuki  cha Igunawapina, upatikanaji wa mashine ya kukamlia asali
katika kituo cha  Igunawapina Kiloleli.

Alisema hadi sasa kuna mipango ya mafunzo kwa vituo vya Sikonge,Kipili
na Kitunda kwa vijana wasiopungua 30 namna ya utengenezaji mizinga ya
kisasa 1,500 ambayitakopeshwa kwenye vikundi vilivypo wilayani humo.

Aidha Selengu anaongeza kuwa bei ya asali imeongezeka toka wastani wa
sh  35,000 kwa ndoo ya lita 20 mwaka 2005, hadi wastani wa sh 80,000
kwa ndoo  ya lita 20 kwa mwaka 2012.

Selengu anasema mafanikio mengine kutokana na kutilia mkazo ufugaji
nyuki  kumepelekea makampuni ya kigeni toka nje Kujitokeza kununua
asali ambapo  makampuni hayo ni,Follow Honey ya Marekani,Honey care,
Honey King (T)Ltd Miombo  Golden Resource.

Changamoto zilizopo

Selengu anabainisha kuwepo kwa changamoto kadhaa ambazo ni uhaba wa
masoko  ya kuaminika kwani wanunuzi wanaofika hapa wanakuja kwa mtindo
wa kulangua  asali na bei haina kiwango maalumu,uhaba wa mavazi ya
kinga kwa wafugaji  (Overall, Bee vail, Gloves) na uhaba wa vifaa vya
kutunzia asali.

Aidha changamoto nyingine ni upungufu wa mvua zinazonyesha kusababisha
upungufu wa chakula cha nyuki na mazao yake,upungufu wa mizinga ya
kisasa  kwa sababu ya ughali wake  uhaba wa mashini za kisasa za
kukamlia asali (Honey Extractor),na uhaba wa  usafiri.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine baadhi ya misitu ya Hifadhi
imevamiwa  kutokana na  shughuli za kilimo, malisho  na makazi ikiwamo
msitu wa  Sikonge, Nyahua na Goweko.
“Juhudi za kuondoa  wavamizi zimekuwa zikifanyika karibu kila mwaka
hasa  katika misitu ya Nyahua, Goweko, Ipembampazi, Iswangala na
Ugunda”.alisema.

Matarajio.

Aidha mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa matarajio yake ni kuendelea
kuwahamasisha wananchi  kuongeza idadi ya mizinga ya kisasa,kuwa na
kiwanda  cha kuchakata mazao ya nyuki ili kuongeza thamani mazao ya
nyuki,asali na  nta hali ambayo itasadia kuwa na masoko ya uhakika
ndani na nje ya nchi.

No comments: