Kipande cha nyama ya Ng'ombe kilichoandikwa maandishi ya Allah kwa lugha ya kiarabu,nyama hii ilinunuliwa Buchani na mara baada ya kufikishwa nyumbani kwao Sheikh Shariff Mikidadi ndipo ikagundulika kipande kimoja kilikuwa na maandishi hayo huku Familia ya ndugu wa Sheikh Shariff wakiwemo kaka zake wakihofia uwepo wa maandishi hayo na hivyo kulazimika kuihifadhi baada kuogopa kuila.
Sheikh Shariff Mikidadi. |
Katika hali inayoendelea kushangaza idadi kubwa ya watu waishio jirani na nyumbani alikozaliwa Sheikh Shariff Mikidadi eneo la Kata ya Kiloleni hapa manispaa ya Tabora ni hii Nyama ya Ng'ombe inayodaiwa kuandikwa jina la Mwenyezi Mungu kwa maana ya Allah kwa Lugha ya kiarabu.
Ama kwa hakika ukikawia kufa utaona mengi,unaweza ukaona na labda ni uchawi lakini hakuna zaidi ya kukubaliana kuwa huu ni MUUJIZA WA MUNGU na hakuna chochote zaidi ya hilo.
Mtandao huu ulipopata tetesi kuhusu tukio la kuwepo kwa Nyama hiyo,ilikuwa ni kazi nyepesi ya kukusanya Kamera zetu na kufika eneo la tukio ili kujiridhisha na MAAJABU HAYO ambayo hata majirani wa eneo hilo wameendelea kustaajabu sana na kushindwa kutambua nini kitakachofuata zaidi baada ya kupatikana kwa nyama hiyo tena kwenye nyumba ambayo alizaliwa mtoto wa maajabu yaani Shekh Shariff mwenyewe.
Ilielezwa na mmoja katika familia ya Sheikh Shariff ambaye ni kaka yake aliyefahamika kwa jina la Abubakari Mikidadi Matongo kuwa,baada ya kununuliwa buchani nyama hiyo ikiwa ni kilo moja na nusu kwa ajili ya kitoweo cha siku hiyo,mara baada ya kuchemshwa jikoni ilitolewa na kuwekwa pembeni ikiwa ni hatua ya kuendelea na mapishi kwa kusubiliwa matayarisho ya viungo vingine, ndipo kipande kimoja kikionesha kujitenga na vingine kilionekana na kikiwa na maandishi hayo yaliyoaminika kuashiria jina la Mwenyezi Mungu yaani ALLAH.
Jambo hili lilizua mshtuko mkubwa ndani ya familia huku wakiitana wao kwa wao na kushauriana nini kifanyike kutokana na Nyama hiyo.
"Kwakweli sisi baada ya kuona hivi tukawa na wasiwasi hata tukafikia uamuzi wa kumfahamisha Sheikh Shariff kwa njia ya simu ambaye kwasasa anaishi Dar-es-Salaam,lakini Sheikh mwenyewe alitutoa hofu kwa kutueleza kuwa huo ni mpango wa Mungu na wala tusiwe na wasiwasi juu ya hilo"alisema Abubakari huku akionesha kipande hicho cha Nyama ambacho hadi sasa kimehifadhiwa kwenye Friji.
UPISHI WA NYAMA YA MAAJABU.
Mke wa kaka yake na Sheikh Shariff anayefahamika kwa jina la Aisha Swalehe au mama Miki ndiye anayedaiwa kupika Nyama hiyo"Chakushangaza nyama hiyo ilikuwa ikichemka kwa staili yake na kwamba ilikuwa ikitoa harufu nzuri wakati ikiwa jikoni na hata wakati tulipoamua kuihifadhi kwenye Friji jambo ambalo bado linaendelea kutushangaza sana"
Bi. Aisha aliendelea kusema kuwa hofu kubwa ilimtanda na hata kufikia hatua ya kutoa taarifa kwa wengine hapo nyumbani ingawa walitaka tukio hilo liwe ni la siri ndani ya familia lakini cha kushangaza zaidi habari zilianza kuzagaa kila kona kwa majirani na hatimaye kuwa dhahiri.
MAJIRANI.
Ingawa tukio hilo lilizua hisia mbalimbali kwa wengi lakini zaidi ya yote majirani wa eneo hilo la Kiloleni wamejiridhisha kama ifuatavyo:-Wapo waliosema kuwa,Kwakuwa Sheikh Sahariff mwenyewe alizaliwa kwa MIUJIZA NA MAAJABU MAKUBWA,tena na kuanza kuhubiri dini ya kiislamu na kufanikiwa kuwabadilisha dini familia yote wakiwemo wazazi wao wote wawili ambao kwa sasa ni marehemu, hivyo kupatikana kwa nyama hiyo iliyoandikwa maandishi ya kiarabu ni wazi kwamba hiyo ni MIUJIZA JUU YA MIUJIZA.
VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU.
Baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wakiwemo walimu wa tafsiri mbalimbali wa lugha ya kiarabu walifika na kushuhudia tukio hilo huku wengi wao wakisema kuwa Mungu mkubwa na kwamba anaonesha uwepo wake katika dunia na hivyo kuwataka waumini wa dini ya kiislamu kushikamana katika kutekeleza maamrisho ya dini yao huenda ikawa ndio siku za mwisho zimefika.
VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU.
Baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wakiwemo walimu wa tafsiri mbalimbali wa lugha ya kiarabu walifika na kushuhudia tukio hilo huku wengi wao wakisema kuwa Mungu mkubwa na kwamba anaonesha uwepo wake katika dunia na hivyo kuwataka waumini wa dini ya kiislamu kushikamana katika kutekeleza maamrisho ya dini yao huenda ikawa ndio siku za mwisho zimefika.
No comments:
Post a Comment