Pages

KAPIPI TV

Sunday, January 20, 2013

SEKONDARI IMEFUNGWA KWA KUKOSA CHOO.

Na Anthony Mayunga-Serengeti.
SEKONDARI ya Mugumu iliyoko kata ya Stendi kuu Mamlaka ya mji mdogo wa
Mugumu wilayani Serengeti imefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na
kutokuwa na choo cha wanafunzi.

Kufungwa kwa shule hiyo iliyoko mjini Mugumu kuna sababisha wanafunzi
1015 wanaosoma shule hiyo kukosa masomo kwa muda usiojulikana .

Ofisa elimu wa sekondari wilaya hiyo  William Makunja amekiri kufungwa
kwa shule hiyo kutokana na kutokuwa na choo na kuwa tatizo hilo ni la
muda mrefu halijafanyiwa kazi.

“Ni utekelezaji wa maagizo ya mkaguzi mkuu wa kanda ambaye aliamuru
ifungwe,tena ilipaswa kufungwa kutokea julai mwaka jana .. na
hawajachukua hatua kama walivyoelekezwa imebidi ifungwe kunusuru
maisha ya watoto”alisema.

Naye kaimu ofisa elimu wilaya shule za msingi Christopher Mossi
alisema uamzi huo julifikiwa baada ya timu hiyo kujiridhisha kuwa
matundu yaliyopo  hayatoshi kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo.

“Shule ina wanafunzi 1015 na kuna matundu 11 ya choo na yote yametitia
hali ambayo ni hatari kwa afya na usalama wao…hitaji la matundu kwa
shule hiyo ni 42 kwa wavulana na wasichana”alisema.

Mkuu wa shule hiyo Magesa Mnyaraga alisema matundu yanayofanya kazi
kwa wasichana ni 4 na wavulana ni 7 hali ambayo haiwezekani kwa idadi
kubwa hivyo.

“Kwa sasa kuna matundu 12 ambayo  yamefunikwa lakini hayana  majengo
yake,hatua ambayo imepelekea shule kufungwa na mamlaka husika baada ya
kujiridhisha”alisema.

Alibainisha kuwa ili kazi hiyo ikamilike inatakiwa tsh,mil.7 ambazo
alidai wameomba  ofisi ya Mkurugenzi mtendaji na kufunguliwa kwake
mpaka wakamilishe ujenzi huo ambao haujulikani utakamilika lini.

Hata hivyo wazazi wa watoto wanaosoma hapo mwaka jana walichangia kila
mmoja tsh,2,500 kwa kazi hiyo ya vyoo ambazo zinadaiwa hazikutosha.

Hata hivyo huenda ikachukua muda kukamilisha ujenzi huo kutokana na
uamzi wa baraza la madiwani kuamua shule hiyo iliyoko kata ya Stendi
mpya kupelekwa kata ya Morotonga ikiwa nje ya mipaka yakiserikali
,wananchi wa mjini wamegoma kuchangia ujenzi huo.

Uamzi huo ambao ulitolewa muda mfupi tu baada ya Chadema kushinda kata
hiyo katika uchaguzi mdogo na kuipeleka shule kata nyingine ulipingwa
na wataalam kwa kuwa ni nje ya mipaka ya kiserikali umeanza kuleta
madhara kwa watoto wanaosoma hapo.

Diwani wa kata ya Stendi kuu Marwa Ryoba alipoulizwa kuhusiana na
tatizo hilo alisema ni matokeo ya siasa zisizokuwa na tija kwa kuwa
kuhamisha shule na kuipeleka kata nyingine hawamkoi yeye bali wananchi
na watoto ambao hawana itikadi hizo.

Hata hivyo amesema tayari wameishawasilisha barua kwa Mkurugenzi na
ngazi zingine na kuwa wanakusudia kulishughulikia kisheria kwa kuwa
uamzi huo ni wa kisiasa ,maana wakazi wa eneo hilo wako kata yake
lakini shule tu inapelekwa kata nyingine.

Mwaka 2008 wilaya hiyo iliandaa harambee ya kuboresha elimu ya
sekondari iliyofanyikia Mwanza ,Mugumu na Arusha na kupata zaidi ya
tsh,mil,200 ,lakini hakuna kilichokwisha fanyika huku usiri wa wapi
zilipo fedha hizo na zinafanya nini ukiwa umetawala.

No comments: