Rais Kikwete akifungua jiwe la msingi ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Tabora hadi Nyahua.
Mkuu wa wilaya ya Uyui Bi.Lucy Mayenga akiwa jukwaani kwa lengo la kuwasalimia wananchi na kumkaribisha Rais Kikwete katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara.
Baadhi ya Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui nao walitoa mpya baada ya kukosa viti vya kukalia katika mkutano wa hadhara wakaamua kukaa chini wakiwa na shauku ya kumsikiliza Rais Kikwete kwenye viwanja vya Chipukizi Tabora mjini.
Mkuu wa wilaya ya Uyui Bi.Lucy Mayenga akiwa jukwaani kwa lengo la kuwasalimia wananchi na kumkaribisha Rais Kikwete katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara.
Baadhi ya Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui nao walitoa mpya baada ya kukosa viti vya kukalia katika mkutano wa hadhara wakaamua kukaa chini wakiwa na shauku ya kumsikiliza Rais Kikwete kwenye viwanja vya Chipukizi Tabora mjini.
Na Lucas Raphael,Tabora
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika ziara yake ya
kikazi mkoani Tabora amesema kuwa kuna haja ya kuundwa Halmashauri mbili katika
wilaya ya Uyui ili kusogeza karibu huduma za maendeleo kwa wananchi.
Akiwahutubia
wananchi wa wilaya ya Uyui katika kata ya Ilolangulu alisema serikali yake
itatekeleza ombi lao la kuwa na halmashauri mbili katika wilaya moja, huku
akiahidi kuiagiza wizara ya ardhi na maendele ya makazi kupima ardhi ya vijiji
hivyo ili waweze kupata hati ya kumiliki ardhi ili waweze kukopesheka katika
taasisi za fedha.
Alisema
hipo haja ya kuwa na halmashauri hizo mbili ilikuwaze kusongeza mahitaji muhimu
kwa wananchi hasa ukizigatia hoja yaumbali mrefu kutioa ilolagulu hadi Isikizya
.
Dkt
kikwete alisema kwamba licha ya umbali huo lakini hipo haja kwa wananchi kuwa
karibu na utawala wao ili kusuma maendeleo kwa wananchi na wapiga kura wa
wilaya ya uyui na jimbo la Tabora Kaskazini.
Akizungumzi
swala la ardhi Rais kikwete alisema kwamba hatamwangiza wazri husika kufika
katika kijiji hicho ili kiweze kupimwa na hatimaye wananchi wa kata hiyo waweze
kupata hati na kupata mikopo katika taasisi za fedha .
Awali
Rais Kikwete alimtaka mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ilolangulu wilayani
Uyui kueleza kero zinazowakabili wananchi wake ambapo mwenyekiti wa serikali ya
kijiji, Ali Magowa, alimweleza kuwa wananchi wanakabiliwa na matatizo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusafiri umbali mrefu kufwata huduma za
kiutawala, kuwa na ardhi ambayo haija piwa na kukosekana kwa maji safi na
salama.
Hata
hivyo alisema kwamba mradi wa milenia mbola bado unahitaji kuendelezwa na
serikali ili kuwasaidia wananchi wa vijiji 16 mabvyo vipo chini ya maradi huo.
Alisema
mradi wa viojiji vya milenia ni muhimu sana kwa
maendeleo ya wananchi wa Tanzania
kwani umesaidia kupunguza umaskini kwa idadi kubwa ya wajkazi wa vijiji hivyo .
Alisema
kwamba haba baada ya mradi huo kulimza muda wake serikali itaendelea kuendeleza
ili kuwa wasaidia wananchi kuendelea kupata mafanikio ya tanfa lao.
Akizungumzia
huduma duni za maji waziri wa maji nchini Prof, Jumanne Maghembe, amesema vijiji
hivyo vitapatiwa huduma ya maji safi
na salama katika kipindi kifupi kijacho.
Alisema
utafiti wa upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo ulifanywa na jaica
ulisitishwa baada ya nchi ya Japan kukumbwa na tetemeko la tsunami ambapo kwa
sasa serikali ya Japan
ipo teari kuendelea na utekelezaji wa mradi huo.
Wilaya
hii ya uyui mkoani Tabora ambayo wananchi wake wanahitaji kusogezewa
huduma za kijamii, kiutawala inatarafa 3, ambazo ni Ilolangulu, Igalula na
Uyui, ina kata 24 na vijiji 120 ikikadiriwa kuwa na watu wapatao 372,761
kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 .
No comments:
Post a Comment