Mh.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia mtoto Abrahamu Omari (miezi 3)
ambaye amebebwa na mama yake mwenye ulemavu wa ngozi anaitwa Amina
Fadhilinyuma ya waziri mkuu ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Reginali
Mengi
ambaye ndiye alianda chakula kwa walemavu katika kukaribisha mwaka mpya 2013.
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana Regina Mengi mtoto wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP .
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anasalimiana na Redds Miss
Tanzania Brigiter Alfred amabaye alikuwa ni miongoni mwa wageni walikwa
katika kushiriki chakula cha mchana na walemavu kilichoanadaliwa na
Mweyekiti wa Makampuni ya IPP Mzee Mengi Picha na Chris Mfinanga
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia walemavu walioalikwa katika chakula cha mchana kilicho andaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni
ya IPP Reginald Mengi katika kukaribisha mwaka mpya wa 2013 waziri mkuu
alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Picha na Chris Mfinanga
…………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema suala la uchangiaji wa
VICOBA kwa ajili ya watu wenye ulemavu linahitaji kupangiwa mkakati
maalum ili kuweza kupata fedha za kutosha kuwapatia mitaji walemavu hatua ambayo itawasidia waweze kujitegemea.
Akizungumza na watu wenye ulemavu jijini Dar-es-salaam wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana kwa ajili ya kuukaribisha mwaka 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mh.Pinda alisema yuko tayari kukaa na Mkurugenzi Mtendaji wa
IPP, Bw. Reginald Mengi ili kuangalia uwezekano wa jinsi ya kutunisha mfuko
wa VICOBA kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
“Bwana Mengi amewasha moto mzuri kwa kuwachangia hawa watu
sh. milioni 100. Nimeambiwa kuwa walianza kwa kujichangisha sh. milioni
17. Najua nami nawajibika kuwachangia lakini itabidi nikae naye tuone
jinsi huduma hii inavyoweza kusambaa na kuwafikia Watanzania wengi
zaidi,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema ili uwe mpango endelevu, wabuni mpango
utakaowajumuisha Watanzania wengi zaidi, wakiwemo wanasiasa, viongozi wa
dini na wengine wengi. “Nia yetu ni kila mwenye nacho achangie ili
kuwasadia wenzetu wawe na miradi ya kujikimu kimaisha kupitia mikopo ya
VICOBA,” alisema.
No comments:
Post a Comment