Pages

KAPIPI TV

Monday, January 21, 2013

IRINGA WAMPONGEZA JK KWA SAFARI ZA NJE YA NCHI


Naibu Meya Bw Ndaki

 

Na  Francis Godwin,
WAKATI vyama  vya upinzani nchini vikipinga ziara  za rais Jakaya Kikwete nje ya nchi Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa mkoani Iringa imepongeza  ziara  za Rais Jakaya Kikwete  nje ya nchi kuwa  imesaidia  kuiwezesha Halmashauri hiyo  kupata  fedha za miradi mikubwa  ukiwemo mradi  wa stendi ya  kisasa pamoja na kuboresha mji  huo zaidi.

Pongezi  hizo zimetolewa leo katika mkutano unaoendelea  na naibu meya  wa Manispaa ya Iringa  Grervas Ndaki   katika mkutano hadhara  wa diwani  wa kata ya Miyomboni  Kitanzini Jesca Msambatavangu  uliofanyika katika viwanja vya soko kuu kwa ajili ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi  ya CCM.

Alisema  kuwa Kupitia mradi wa benki ya dunia  kwa  jitihada za Rais Kikwete  Manispaa ya Iringa imepata  msaada  wa kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya shughuli  hizo pamoja na kujenga barabara  za lami katika mitaa ya mji  wa Iringa na maeneo ambayo yalikuwa yanaongoza  kwa kero ya barabara.

Ndaki  alisema  kuwa kutokana na  ziara  hizo  za Rais Kikwete nje ya nchi  zimekuwa ni mafanikio makubwa kwa Halmashauri hiyo  kupata msaada  huo  wa  fedha kutoka benki ya dunia .

Hata  hivyo  alisema  kuwa  bado manispaa ya  Iringa  imejiwekea mikakati ya  kuboresha mji kwa usafi ikiwa ni pamoja na kununua magari  ya  kisasa ya  kubeba takataka pamoja na kununua madampo ya  kuhifadhia taka zaidi ya 100.

Pia  alisema  kuwa Manispaa ya Iringa imetumia kiasi cha shilingi Milioni 581 kununua greda katika Halmashauri ya manispaa ya Iringa  kwa ajili ya kuboresha miundo  mbinu katika mji wa Iringa. la Manispaa ya Iringa.

Aidha  alisema Manispaa ya Iringa imekusudia  kuboresha  pia soko la Kihesa pamoja na kujenga barabara ya Kitwiru ,Ruaha na Isakalilo ambazo zitatengenezwa kwa kiasi cha shilingi milioni 73.

Huku milioni 92.2 zinategemewa  kuboresha barabara  za Kitanzini ,Ilala Makorongoni  na maeneo mengine  barabara ambazo zinaongoza kwa ubovu.

Kuhusu  taa zinazowekwa katika mtaa wa Kitanzini na stendi  kuu ya Manispaa ya  Iringa  alisema  kuwa taa zinazowekwa na mfanyabiashara mmoja mjini Iringa na si vinginevyo .

Alisema  kuwa  Mji mzima  wa Iringa  kuwashwa taa  ili  kupunguza tatizo la vibaka  kupora  watu majira ya usiku.
Kuwa taa hizo gharama zote ni za mfanyabiashara  huyo na kuwa yeye atapewa  jukumu la kuweka mbao za matangazo katika taa zote.
Manispaa ya Iringa yajipongeza  kwa  kuendelea  kuongoza matokeo ya darasa la  saba kimkoa kwa miaka  saba mfululizo  sasa yapongeza  walimu wa  shule  za msingi kwa  kazi nzuri kwa  kuwezesha  wanafunzi asilimia 90 kufaulu kwenda sekondari.
Shule  za sekondari zipo 13 na wakati  wowote  kuanzia mwezi huu idadi ya  shule za sekondari kuongezeka na kuwa 14  kutoka 13 za  sasa.

Hata  hivyo  alisema  kuwa tatizo la  walimu katika Manispaa ya Iringa si tatizo kwa  sasa kwani  waliopo wanatosha ila tatizo ni  walimu  wa masomo ya  Sayansi na mahabara bado ni tatizo kubwa.
Kwa  upande  wake  diwani  Msambatavangu  alisema kuwa akiwa kama diwani wa kata  hiyo na mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa atahakikisha anaendelea  kueleza  utekelezaji  wa Ilani ya CCM kila  wakati na kuwa suala la malumbano ya kisiasa  kamwe halitatakiwa katika utendaji  wake.

Alisema kuwa  suala  kubwa ni kutekeleza ilani ya CCM kwa pamoja  kuanzia mbunge wa jimbo  hilo mchungaji Peter Msigwa (chadema(pichani ) na  madiwani  wote na sio kuendeleza malumbano yasiyokwisha ya vyama.
Msambatavangu  alisema kuwa kwa kawaida katika nchi  yeyote  duniani ilani  ya  chama  kinachoshika dora ndiyo inayotekelezwa na sio  vinginevyo.
Alisema  kuwa ilani ya  CCM inazungumzia  suala  zima la uchumi  wa kisasa na yenye  kuwawezesha   wananchi  kuweza  kujitegemea  zaidi .

No comments: