Pages

KAPIPI TV

Tuesday, December 18, 2012

NDEGE YA TANAPA ILIVYOANGUKA MPANDA



Askari akiangalia ndege aina ya Cessina yenye namba 5 H F25C 182 ambayo ina uwezo wa kubeba abiria wanne,ikiwa imeanguka nje kidogo ya Uwanja wa ndege Mpanda mkoani Katavi kando ya Mto Nsemulwa juzi. Ndege hiyo ilipata hitilafu ikiwa na rubani ambaye alinusurika.  


NDEGE ndogo ya abiria mali ya Hifadhi ya Taifa ya Tanapa  yenye uwezo wa kubeba  watu  wanne aina ya C 182, imeanguka katika  eneo la Kasimba  umbali wa kilometa moja  kutoka katika  Uwanja wa Ndege wa Mpanda  uliopo katika Mkoa wa Katavi  na kumjeruhi rubani wa ndege hiyo.


Akizungumza na vyombo vya habari, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Maulid  Mohamed alisema ajali  hiyo  ilitokea jana  majira saa 10 .55 jioni  katika   eneo la Kasimba lililopo ndani ya Kijiji  cha Nsemlwa   wilayani hapo.


Mohamed aliitaja ndege hiyo iliyoanguka na kusababisha majeraha kwa rubani aliyetajwa kwa jina la Adam Athuman Kajwaa kuwa  ni aina ya C182.

Mohamed  alieleza kuwa  ndege  hiyo   ilikuwa imetoka  katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikielekea  katika Hifadhi ya Wanyamapori  ya Katavi.   

Hata hiyo alisema kuwa ajali hiyo  ilitokea   umbali wa  kilometa  moja na  nusu  kutoka Uwanja wa Ndege wa Mpanda  mara  baada  ya  kuondoka  katika uwanja huo ambapo imeharibika sana sehemu ya bawa lake na upande wa injini.

Meneja wa uwanja  huo wa ndege  alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo   cha ajali  hiyo  kilitokana na kufeli kwa  injini  ya ndege  na kuwa rubani wa ndege hiyo   alipata msaada  wa kuokolewa na  wananchi  waliokuwa  wakifanya  shughuli  za  kilimo  kwenye  mashamba.

Mmoja wa  wa mashuhuda wa tukio hilo Credo Mwanisenga   alieleza  kuwa wakati   akiwa  anafanya shughuli  zake  za kilimo  ghafla  aliona  ndege  hiyo ikiwa  angani  ikizimika  na baada ya  muda  mfupi   ikaanguka   jirani  na mti wa mwembe.

Hata hivyo alisema kuwa zoezi la kumuokoa rubani huyo lilichukua muda kuanza kutokana na mti wa mwembe  kuwa na nyuki wengi.

Hata hivyo  alisema mara baada ya   kufanikiwa kumtoa  rubani  huyo,   huku akiwa  amepata  majerahi makubwa sehemu ya  uso  na maumivu  sehemu ya kifua   na kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu zaidi.

Pia akiwa anakohoa damu,  rubani huyo aliwahishwa  haraka katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda baada ya kupata  msaada wa gari la meneja wa uwanja wa ndege aliyefika  eneo   la tukio.

No comments: