Pages

KAPIPI TV

Wednesday, December 5, 2012

MWANDISHI WA HABARI APIGWA RISASI DAR.

                                                                 
Na Francis Godwin.
Mwanahabari mwingine  mkoani Dar es Salaam apigwa  risasi na askari  polisi ambao  wanadaiwa  kuwa  walikuwa  wakimsaka mtuhumiwa  wa ujambazi  mwanamke na kuishia kumpiga mwanahabari  huyo mwanaume  Bw  Shaban Matutu wa gazeti la Tanzania  Daima.

Tukio  hilo limetokea jana majira  ya saa 2 usiku  jijini  Dar es Salaam ambapo askari  hao walipofika  nyumbani  kwa  mwanahabari  huyo na  kumgongea mlango na  wakati akifungua mlango ndipo

 Matutu amepigwa risasi na Polisi, ambao wanadaiwa walikuwa wanamtafuta mhalifu ambapo katika zoezi hilo, walienda na kugonga chumbani kwa Mwandishi huyo, kabla ya kutwanga kwa risasi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mara baada ya tukio hilo, mwandishi huyo amekimbizwa hospitali ya Mwananyamala ambako anaendelea kupatiwa huduma ya haraka na inaelezwa kuwa, amejeruhiwa lakini hali yake si mbaya sana
Habari zaidi zitakujieni

Taarifa za uhakika na ambazo zimethibitishwa­ zinaeleza kuwa jana usiku polisi mwenye silaha, aina ya bastola alimjeruhi begani kwa risasi, mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Shaaban Matutu.


Risasi bado imenasa kwenye bega lake hadi sasa Matutu alipigwa risasi nyumbani kwake Kunduchi, Dar es Salaam wakati askari walipovamia nyumba yake kwa madai kwamba kuna kibaka aliingia kujificha nyumbani hapo. Hivi sasa Matutu anatibiwa Mwananyamala hospitali, lakini amepewa rufaa kwenda Muhimbili.


Mwenyekiti  wa  jukwaa la wahariri Tanzania Bw Absalom Kibanda, ambaye amefanya jitihada za kumuhamishia Matutu Muhimbili, anasema hali ya Matutu siyo nzuri na kwamba wanajipanga kwenda Muhimbili kuona iwapo risasi hiyo itaondolewa mwilini.


Hata  hivyo  Kibanda ameeleza  kusikitishwa kwake ni  vitendo vya uvunjifu wa amani dhidi ya  wanahabari nchini Tanzania ambavyo  vimeendelea kufanywa na jeshi la  Polisi nchini na kutaka polisi  waliofanya  hivyo  kuchukuliwa hatua  kali.


Alisema wakati Taifa likiwa bado katika majonzi ya  mauwaji ya  kinyama ya Mwandishi wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi leo  tunashudia tena unyama mwingine dhidi ya  mwanahabari  huyo.


Hivyo  iwapo jeshi la  polisi litakosa majibu juu ya sababu ya  kumpiga risasi mwanahabari  huyo ambaye hata  hivyo hakuwa mlengwa katika msako wao  wa kumsaka mtuhumiwa wa ujambazi ambae ni mwanamke basi itafika  sehemu  wanahabari nchini  watalichukulia jeshi la polisi ni maeneo ya hatari kwao

 

No comments: