Na Berensi Alikadi.
SIKU Chache baada ya vyombo
vya habari kuandika habari za mbunge wa jimbo la Tarime Nyambari Nyangwine kuwa
amelisusia jimbo lake
kwa muda wa miezi
sita,mbunge huyo ameibuga na kusema habari hizo siyo za kweli.
Akiongea na waandishi wa
habari jana jijini Dare-salaam,mbunge amesema kuwa taarifa hizo si za kweli
bali zilikuwa zinalenga kumchafulia jina lake.
Nyambari alisema kuwa
wananchi wa Tarime lazima watambua kuwa mbunge yeyote ni mwakilishi wa nchi
nzima na kwamba hata vikao vya bunge vinapoisha huingia katika majukumu mengine
ambayo ni ya kitaifa na kwamba suala la kuchelewa kwenda jimboni siyo la
makusudi hivyo wananchi lazima watambue hilo.
‘’ Mimi niwaambie hizo ndizo
siasa zetu za Tanzania
watu wako makini kwa kuandika majungu,wiki iliyopita nilikuwa jimboni na
nimefanya mikutano mingi na nimetembelea vijiji vingi na nimekuwa nikifanya
hivyo kila mara sasa aliyesema kuwa nimekimbia jimbo huyo ana yake’’alisema
Nyangwine.
Akizungumzia mauji ya
wananchi yanayoendelea kufanywa na askari polisi katika vijiji vilivyo kando
kando ya mgodi wa Nyamongo,mbunge huyo amesema kuwa wananchi wanapaswa kufuata
sheria lakini polisi waache kuonea wananchi maana sasa wananchi wamechoka
kuonewa.
Mbunge huyo aliutaka mgodi
huo kuwalipa fidia wananchi wote wanaodai kwani madai hayo ni mali yao na
kwamba wasipofanya hivyo yeye atawaongoza wananchi katika kudai haki yao ambapo amesema kuwa hapo lazima patachimbika kama hawatalipa
Alifafanua kuwa mgodi ulisema
kuwa umetenga kiasi cha dola million tano kwa ajili ya kuendeleza wachimbaji
wadogo wadaogo wailoko katika maeneo hayo lakini hadi sasa hajatekeleza hivyo
ni vyema wakafanya walichoahidi.
Kuhusu taarifa za kuuzwa kwa mgodi wa Barrick kuuzwa
kwa kampuni ya Kichina mbunge huyo amesema kuwa yeye hana taarifa ya kuuzwa kwa
mgodi huo na kwamba hata kama umeuzwa
anachotaka ni wananchi wake kulipwa fidia.
No comments:
Post a Comment